LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 5, 2020

Video: KISWAGA: WAPINZANI HAWAFAI KUCHAGULIWA WALIKIMBIA BUNGENI


Mgombea Ubunge Jimbo la Magu kupitia CCM, Boniventura Kiswaga akimwaga sera nzuri za CCM  katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Salama ambapo aliwaomba  wananchi kumpigia kura yeye, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli na wagombea udiwani wa chama hicho
Ni burudani kwa kwenda mbele

 

Mgombea Ubunge Jimbo la Magu kwa tiketi ya CCM Ndg.Boniventura Destery Kiswaga ameendelea kuchanja mbuga katika kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 28,2020. 

 Kiswaga akiwa katika mkutano wa kampeni katika kijiji cha Salama amewaomba wananchi kutojaribu kuwachagua wapinzani katika ngazi yoyote ‘ Ndugu zangu wapinzani hawa juzi Dunia ilipoingia kwenye janga la Covid -19 Wabunge wa upinzani wote walilikimbia Bunge wakihofia kufa, Tulibaki wabunge wa CCM ndiyo tumepitisha Bajeti ikiwemo hii ya Uchaguzi.’ Alisema Kiswaga. 

 Aidha Kiswaga amesisitiza kuwa Wapinzani hawana dira yoyote, bali ni wapiga kelele na watu wasiokuwa na shukrani nawafananisha na watu ambao siku zote wao huwashukuru wafu. 

Hawana kumbukumbu juu ya kazi njema na nzuri zilizofanywa na Serikali ya Rais mpendwa Dk. John Magufuli.Nawaomba kura zote tuichagua ccm ndiyo ina Ilani nzuri na yenye dira ya maendeleo kwa Taifa letu. ‘Tumetekeleza kwa kishindo na Tunasonga mbele kwa pamoja’ 

 CHAGUA CCM MITANO TENA!!

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages