LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 28, 2020

RAIS MAGUFULI, MKEWE WAPIGA KURA CHAMWINO DODOMA

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais John Magufuli na mkewe Janet wakipiga kura Chamwino, Dodoma asubuhi hii ya Oktoba 28,2020.


Baada ya kupiga Dk. Magufuli amesema,

"Nawapongeza Watanzania kwa kuiona siku hii ya leo muhimu, naona maandalizi yalikuwa mazuri nimepiga kura mimi na mke wangu".

"Nasisitiza amani tuendelee kuitunza Watanzania kwa sababu kuna maisha baada ya uchaguzi"

Magufuli anawania muhula wa pili.



Dk. Magufuli na mkewe wakiwa kwenye foleni wakisubiri zamu yao ya kupiga kura.

Dk. Magufuli akiingia kupiga kura katika Kituo cha kupigia kura cha Chamwino kilichopo na Ikulu.

Mama Janet akipiga kura

Dk. Magufuli akiwa eneo la siri la kupigia kura



Dk Magufuli akionesha dole  baada ya kupiga kura.
Dk. Magufuli akiweka wino kwenye kidole ikiwa ni ishara ya kwamba ameshapiga kura na haruhusiwi kwenda kupiga kura sehemu nyingine tena.
Dk Magufuli akizungumza na vyombo vya habari baada ya kupiga kura.






No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages