LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 31, 2020

RAIS DK. MAGUFULI KUKABIDHIWA KESHO HATI YA USHINDI WA URAIS 2020 JIJINI DODOMA


Rais Dk. Magufuli akiwa na Mgombea mwenza wake, Samia Suluhu Hassan


Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wanatarajiwa kukabidhiwa rasmi Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais kesho Novemba Mosi, 2020.

Taarifa zimesema hafla hiyo itafanyika kuanzia saa moja asubuhi katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zilizopo katika Jengo la Uchaguzi House eneo la Njedengwa jijini Dodoma.

Dk. Magufuli alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jana  kuwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi mno  wa kura 12,516,252, akifuatiwa na Tundu Lisu wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA) mwenye kura  1,933,271 huku  Bernard Membe kutoka Chama cha ACT-Wazalendo akiwa amepata kura 81,129.

Ushindi wa Dkt.Magufuli umepatikana baada ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu uliofanyika October 28,2020 huku jumla ya waliojiandikisha ni 29,754,669, na kura halali zilizopigwa ni 14,830,195 huku kura 261,755 zikikataliwa.

Baada ya kukabidhiwa Cheti hicho Rais Mteule Dkt.John Magufuli na Makamu wake watasubiri kuapishwa rasmi

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages