Bibi mkai wa Kigwe, Bahi, akiibusu picha ya Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli. Picha hiyo aligawiwa na Okash.
Okash akma kawaida yake akiomba kura kwa unyenyekevu katika moja ya mikutano ya kampeni Jimbo la Bahi.
Akioneshana dole gumba alama ya CCM na mmoja wa wakazi wa Kigwe, Bahi.
Okash akigawa picha Dk Magufuli sambamba na kumuombea kura.
Akiomba kura kwa unyenyekevu katika moja ya vijiwe Jimbo la Bahi.
Okash akiwa na akina mama akiwapatia maelekezo ya jinsi ya kupiga kura kwa CCM.
Akiongea na mmoja akina bibi ambapo pia alimpatia picha ya Dk Magufuli.
Na Mwandishi Wetu, Bahi.
MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima Okash ametumia ubunifu kutoa elimu kwa wapiga kura kwa kuchora chini kwenye udongo kaboksi ka kupigia kura na kuwaelekeza wananchi jinsi ya kupiga kura Jumatano ijayo Oktoba 28.
Okash alitoa elimu hiyo alipokwenda Jimbo la Bahi kufanya kampeni ya kuwashawishi wananchi kupiga kura za mafiga matatu kwa CCM, yaani Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli, Mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Kenneth Nollo na wagombea udiwani wa chama hicho.
Alifanya kampeni ya nyumba kwa nyumba ambapo ilimwezesha kukutana na kada mbalimbali wakiwemo wazee, vijana, akina mama, wajasiriamali, waendesha bodaboda na wakulima ambao aliwaelezea umuhimu wa kwenda kupiga kura na jinsi ya kupiga kura siku hiyo ya Jumatano Oktoba 28.
Alipokuwa katika Kata ya Kigwe Kichangani, Okash aligundua baadhi ya wananchi hawaelewi jinsi ya kupiga kura, ndipo akaamua kuwaelimisha kwa kuchora mfano wa kisanduku chini kwenye udongo na kuwaelekeza jinsi ya kutia alama ya vema katikati.
"Pamoja na kufanya kampeni ya kuwaombea kura wagombea wa CCM, nilipata fursa pia ya kuwaelekeza jinsi ya kupiga kura, kwa vile nilikuwa sina karatasi la mfano kupigia kura, niliamua kuchora chini kaboksi ka kupigia kura na kuwaonesha alama ya vema inavyotakiwa iwe ndani yake, lakini kwa wasiojua kusoma niliwambia wataona alama ya CCM ya jembe na nyundo kwa wagombea wa CCM," alifafanua Okash.
Anasema baada ya kutumia njia hiyo rahisi wengi walimuelewa na kuahidi Oktoba 28, watawahi mapema kwenda kwenye vituo kupiga kura na kurejea nyumbani kusubiri matokeo lakini vilevile kujiepusha na shari endapo itatokea.
Pamoja na kujikita kutoa elimu hiyo ya jinsi ya kupiga kura, anasema kila kundi alilokutana nalo alijitahidi kuwaelezea uzuri wa sera ya CCM na mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano inyoongozwa na D. Magufuli.
Pia Okash, alielezea mambo mazuri yaliyomo kwenye Ilani ya CCM 2020-2025 ana kwamba ili yatekelezwe ipasavyo, basi hawana budi kuwapigia kura wagombea wa CCM ambao ni Mgombea Urais, Dk. Magufuli, Mgombea ubunge Jimbo la Bahi, Nollo na wagombea udiwani wa chama hicho.
Baada ya kampeni za nyumba kwa nyumba, Okash alikwenda kuhudhuria mkutano wa kampeni wa hadhara wa CCM ambapo aliwanadi wagombea hao CCM na kuwahimiza Jumatano ijayo Oktoba 28,kuwahi mapema vituoni kupiga kura na kurejea nyumbani.
Akielezea utendaji wa Okash, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dodoma, Billy Chidabwa ambaye jana alikuwa naye katika kampeni Jimbo la Bahi, anasema kuwa ni dada anayejituma kikweli kweli kwenye kazi, si mtu wa kusukumwa, hata kabla ya kuanza vikao anautumia muda mfupi alionao kusambaza vipeperushi mitaani sambamba na kuwaombea kura wagombea wa CCM.
"Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Okash ni dada anayejituma kweli kweli kupambania kura za wagombea wa CCM, nimekuwa nikikutana naye maeneo mengi ambayo sikutegemea kama angefika tena pembezoni kabisa ya vijiji kama kule Chamkoroma Kongwa, anajua sana kufanya kampeni kuanzia za nyumba kwa nyumba, mikutano ya ndani na ya hadhara.
Okash yupo makini na kazi yake, anajua anachokifanya, anafanya kampeni kutoka moyoni na watu wanamuelewa vizuri, hataki muda upotee bure, muda wa kusubiri vikao yeye huchukua vipeperushi na kuvisambaza mitaani sambamba na kuwaombea kura wagombea wa CCM, kwa ufupi ni mtu Serious na kazi yeke," alisema Chidabwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇