Serikali ya Tanzania inatazamiwa kutuma helikopta na ndege katika Mlima Kilimanjaro kusaidia kuuzima moto unaoendelea kuwaka kwa siku ya saba sasa.
Hayo ameyasema Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangala baada ya moto kuendelea kuwaka katika mlima huo .
Jana Waziri Kigwangala alitangaza kuwa wameweza kuudhibiti moto huo, lakini baadaye moto huo ulisaambazwa zaidi na upepo uliovuma katika mlima huo.
Katika ujumbe wake wa Twitter Waziri Kigwangala amethibitisha kuwa moto unaendela kuwaka katika mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.
Unaweza pia kutazama:
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇