LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 14, 2020

MCHINGA KUCHELE, MNEC JAPHARI KUBECHA AENDELEA KUMNADI MAMA SALMA KIKWETE JIMBONI


Jumanne, Oktoba 13,2020


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Japhari Kubecha Mghamba jana aliendelea kumnadi kwa nguvu zote Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Mchinga, Mama Salma Kikwete kwa kuzunguka katika Vijiji vilivyopo katika Kata za Mvuleni na Kilolambwani katika jimbo hilo.


Kabla ya mikutano ya hadhara MNEC Kubecha aliweza kukutana na wanawake katika Kata ya Kilolawambwani na kumuombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli, Mama Salma Kikwete na Diwani wa CCM, akiwasisitizia wanawake hao kuhakikisha siku ya Oktoba 28, 2020 wajitokeza kwa wingi na kumpigia kura Dk. Magufuli na pia kumuunga mkono mwanamke mwenzao Mama Salma kwa kumpa kura za kutosha kuibuka na ushindi mnono wa kiti cha Ubunge.


MNEC Kubecha aliendelea na zoezi la kutafuta kura ambapo aliweza kushiriki katika mkutano wa Hadhara kwenye kata ya Kijiji cha Kijiweni na kuwaomba wananchi wamchague Dk. Magufuli, Mbunge Mama Salma na Diwani wa CCM na kuwasisitiza kwamba serikali imejipanga kikamilifu katika Ilani ijayo ya 2020-2025 kuleta maendeleo ya kutosha kwenye jimbo la Mchinga na Taifa kwa jumla.


Katika mikutano hiyo MNEC Kubecha amewasisitiza wananchi wasifanye tena makosa wamchague Mama Salma Kikwete maana anatosha na ana uchungu na wananchi wa Jimbo la Mchinga na amejipanga vyema kuhakikisha analeta maendeleo ya kutosha kwenye jimbo hilo.


Aliwaomba wananchi wapuuze porojo zinazopigwa na wagombea ubunge wa vyama vya upinzani katika jimbo hilo kwa kuwa hazina tija na wamekosa sera hivyo hakuna haja ya wananchi kuwachagua badala yake wachague sera bora nazo ni  za CCM tu zitakazosimamiwa kwa uhakika na Dk. Magufuli, Mama Salma Kikwete na Madiwani wa CCM.


Katika mikutano hiyo Mama salma aliwaomba wananchi kumchagua Oktoba 28, huku akiwaahidi kwamba atasimamia vyema Ilani ya CCM 2020-25 ambayo imelenga kuleta maendeleo makubwa katika jimbo la Mchinga na nchi nzima  na kuwaambia kuwa wakimchagua atahakikisha anatatua changamoto zote zinazowakumba wananchi ili kusudi Mchinga iwe mpya kwa maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali.

TASWIRA KATIKA PICHA👇










No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages