LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 16, 2020

MASLAHI YA TAIFA HAYABEZWI ZAIDI YA KULINDWA


 

Mtu Yoyote anayebeza Maendeleo Yetu Kama Taifa Maana Yake anabeza Maslahi ya Taifa la Tanzania.Mtu anayebeza Miradi Mikubwa ya Kimkakati na Kusema haya ni Maendeleo ya Vitu huyo anabeza Maslahi ya Watanzania Wote"Public Interests"

Maslahi ya Taifa"National Interest" hubebwa na dhana Kuu Kubwa tatu ambazo ni Uzalendo,Nidhamu Uadilifu.


MASLAHI YA TAIFA NI NINI?

Kwa tafsiri rahisi kabisa Maslahi ya Taifa ni Mambo Yote ambayo yanalinda Mustakabali wa Taifa fulani Kiuchumi,Kisiasa na Kiutamaduni.

Maslahi ya Taifa hujengwa Katika Msingi wa "Maslahi ya Wengi" Yalindwe na Maslahi ya Wachache Yafate.

Maslahi ya Taifa pia hujengwa Katika Msingi wa Maendeleo ya Wengi Yaanze Kuliko Maslahi ya Wachache.


MASLAHI YA TAIFA NI YAPI!

Maslahi ya Taifa hujengwa Kwenye  Kulinda na Kutumia  Rasilimali za Taifa kwa Maslahi ya Wengi"Public Interests".

Mwisho wa Siku Maslahi ya Taifa Uambatana na Kulinda Uhuru"State Sovegnity" na Umoja wa Taifa"National Unity".

Lakini pia Maslahi ya Taifa Ujengwa Katika Uwezo wa Taifa Kutafuta Maslahi yake Nje ya Mipaka kupitia Mikataba ya Kimataifa"Treaties",Biashara ya Kimataifa 

Wakati Mwingine Kushiriki Shughuli za Kiulinzi na Usalama Nje ya Nchi.Kwa Mfano,hili Kulinda Maslahi ya Nchi,Tanzania italazimika Kulinda amani ya Nchi za  Maziwa Makuu ili Kuhakikisha haileti hadhari za Kivita.

Uwepo wa Wakimbizi wa Burundi Katika Tanzania kwa Miaka Zaidi ya Kumi Ungeweza Kuhatarisha Maslahi ya Tanzania Kiusalama Kuliko Kama ambavyo Burundi Ingekuwa na amani.

MASLAHI YA TAIFA MLINZI WAKE NI NANI?

Mlinzi Namba Moja wa Maslahi ya Taifa ni Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Nchi ya Tanzania. Mtu Huyu Uapishwa Kuyalinda na Kuyatetea Maslahi hayo ya Taifa dhidi ya Adui wa Ndani au Adui wa Nje.

Hili Rais aweze Kuyalinda Maslahi hayo ni lazima Rais huyu awe na tabia za Kipekee Tatu Kubwa. Moja,MZALENDO,Mzalendo ni Mtu ambaye Yupo tayari kufa kwa ajili ya Kulinda Maslahi ya Taifa lake"Uhuru,Uadilifu,nidhamu,heshima,Umoja,Maadili na tunu za Taifa bila aibu Yoyote.

Mbili,MUADILIFU,Madilifu ni Mtu ambaye anayashinda Maslahi yake binafsi,ya Ndugu Zake au Jamaa zake kwa ajili ya Kulinda Kwanza Maslahi ya Wengi"Public Interests".


Watu hawa huweza kuzishinda tamaa Zao Kifedha,Kimadaraka,na Kimwili pia kwa ajili ya Manufaa 

ya Wengi au ili Kuweza Kulinda haki za Wengi.


Tatu, NIDHAMU,Nidhamu pia ni Sehemu ya Sifa Kuu ya 

Rais Mzalendo. Nidhamu ni hali ya Kusimamia Mambo 

Mliyokubaliana Kwa Kuzingatia Mda na Ubora wa huduma 

Unayotoa Kwa Watu.


Rais anapaswa Kulinda Kiapo Chake Cha Kikatiba Cha 

Kulinda Maslahi ya Taifa bila Kuyaonea aibu dhidi ya 

Wanaotafuta Kuyabomoa Maslahi hayo.


WANANCHI au Raia ni Kundi la Pili Katika Kulinda 

Maslahi ya Taifa kwa Kuhakikisha Wanafanya Kazi Hili 

Kupiga hatua za Maendeleo Katika Nyanja Zote za 

Maendeleo.


MASLAHI YETU KAMA TAIFA NI YAPI?


Amani Yetu Kama Taifa ndio Maslahi Yetu,Uhuru Wetu 

Kama Taifa ndio Maslahi Yetu,Rasilimali Zetu Kama 

Taifa ndio Maslahi Yetu,Umoja Wetu Wetu ndio Maslahi 

Yetu Kama Taifa,Tunu Zetu Kama Taifa ndio Maslahi 

Yetu,Miradi Yetu Kama Taifa ndio Maslahi Yetu na Kwa 

Ujumla Maendeleo Yetu Kama Taifa ndio Maslahi 

Yetu."Common Interests".


KUMDHARAU RAIS NA AMIRI JESHI WETU NI KUTUKANA MASLAH YETU KAMA TAIFA.


Tunasema Rais ndio Mlinzi Namba Moja wa Maslahi ya 

Nchi,Rais Utumia Vyombo Vyake vya Dola Kulinda Maslahi 

hayo.


Kwahiyo Kumsema Vyovyote Rais Kwa lengo la Kumvunjia 

heshima Mfano Juzi Mh. Tundu Lissu Mgombea Urais Kwa 

tiketi ya Chadema akiwa Kwenye Mkutano Wake wa Kampeni 

alisikika akisema.."......Rais Magufuli anafikiri Sisi ni Washamba Kama Yeye.....Benki gani Utapata Mkopo Kwa 

Kitambulisho kile....hakina Picha,hakina Jina.......".


Kiufupi Tundu Lissu anahatarisha Maslahi ya Taifa na Asije akashangaa Walinda Maslahi hayo "Wakimrukia".

Rais Bora wa awamu ya tano lazima aweze kuyajua na 

Kuyalinda Maslahi ya Taifa lake.


KURA Yako Kampeni Mgombea anayelinda Maslahi hayo Kwa ajili ya Vizazi Vya leo na Kesho,Rais John Pombe Magufuli anakuhakikishia Ulinzi wa Maslahi hayo.


Chagua John Pombe MAGUFULI,Chagua Chama Cha Mapinduzi, Chagua Maendeleo.


William Peter Ndilla

Sumve, Mwanza.

+255759929244

October 14,2020.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages