LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 27, 2020

KWA ALIYOYAFANYA JPM NCHI ISINGEINGIA KWENYE UCHAGUZI ,FEDHA ZILIZOTENGWA ZINGEPELEKWA KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

 



Na.Mwandishi Wetu,Dodoma 

ALIYEKUWA mtia nia katika kura za maoni katika mchakato wa kura za maoni katika  jimbo la Kongwa Samwel Chimanyi amesema,kutokana na  aliyoyafanya Rais Dkt.John Magufuli ,kulikuwa hakuna haja ya kufanya uchaguzi Mkuu mwaka huu na badala yake viongozi wa vyama vyote vya siasa wangekubaliana kutosimamisha wagombea na kumpa ridhaa Dkt.Magufuli kuendelea katika kipindi cha pili cha miaka mitano.

Kauli hiyo ameisema Leo jijini Dodoma 

Chimanyi amesema kuwa mambo mengi ambayo  yalikuwa yakipigiwa kelele na vyama vya upinzani Dkt.Magufuli ameyafanya.

Hata hivyo amesema kuwa viongozi wote wa vyama vya siasa wangekubaliana Dkt.Magufuli aendelee kuongoza kumalizia kipindi chake cha miaka mitano, nchi isingeingia katika uchaguzi na ingeokoa mabilioni ya fedha.

“Licha ya kuwa ni haki yao kikatiba kusimamisha wagombea kutoka katika vyama vyao lakini wangekuwa wazalendo tu kumuunga Dkt.Magufuli mkono ili aendelee na kukamilisha mambo ambayo ameshaanza.” Amesema Chimanyi

Chimanyi amesema kuwa ,Dkt.Magufuli ambaye amegombea tena nafasi ya urasi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),amefanya mambo makubwa hapa nchininkwa ajili ya Maendwleo ya watanzania .

Aidha amesema kuwa ,licha ya kujenga miradi mikubwa lakini pia kiongozi huyo ameweza kud



hibiti rushwa nchini lakini pia kuwakabili mafisadi ambao walikuwa wakiitafuna nchi kwa kula mabilioni ya fedha za Serikali na kujinufaisha wao binafsi badala ya kuwanufaisha watanzania.

“Tuseme ukweli Dkt.Magufuli katika mambo haya amefanya kwa vitendo,Licha ya kuwa bado hayajaisha kanisa lakini akipata nafasi nyingine atayasimamia kwa nguvu na kuyapunguza kwa kiasi kikubwa kama siyo kuyamaliza kanisa.” Amesisitiza

 Kufuata hali hiyo Chimanyi amewaasa watanzania kumchagua kiongozi mpenda maendeleo na mwenye uwezo wa kuwamudu hata walio chini yake.

“Ninafahamu kila mtanzania ana haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi anayemtaka,ndio maana nawasihi watumie haki hiyo vizuri kwa kumchagua kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza na kuwaletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.” Amesema na kuongeza

“Pia watanzania wamchague Rais atakayeondoa mafisadi,nchi hii ilitawaliwa na rushwa na mafisadi lakini katika uongozi wa serikali ya awamu ya tano imejitahidi kuyapunguza haya mambo,mafisadi wamerudisha fedha nyingi za Serikali , na nina uhakika akipata ridhaa nyingine mambo hayo yanaweza kumalizika kabisa.”

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages