LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 24, 2020

KISWAGA-AUSIMAMISHA MJI WA MAGU, MAELFU WAMPONGEZA KUTATUA KERO YA MAJI.




 Mgombea ubunge jimbo la Magu kwa tiketi ya CCM Ndg.Boniventura Destery Kiswaga zikiwa zimesalia siku chache ili kufanyika uchaguzi mkuu wa Octoba 28,2020. akiwa katika kampeni wakazi wa mamlaka ya mji wa Magu wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya sabasaba.

Kiswaga amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi, ‘Mmetisha leo hii ni dalili kuwa mnayo imani kubwa kwa Wagombea wa CCM, Mimi nawahakikishia kuwa Maji tumeleta na tumesambaza kilomita 64, tumeomba tena kwa Dr.John Pombe Magufuli na tumekubaliwa mtandao wa maji utaongezwa kwa kilomita 24. Pia tutaendelea kuboresha sekta za Afya, Elimu,Kilimo,Barabara na Miundombinu’ Alisema Kiswaga.

Kiswaga ameendelea kufafanua kuwa mwaka 2015 wakati anachaguliwa Magu ilikuwa na mtandao wa barabara km 391, wameongeza mtandao wa barabara na kufikia zaidi  km 1500, Afya tumeleta X-ray mashine ya kisasa na Utral sound mashine na ujenzi wa vituo vya afya vitatu, jengo la OPD na Zahanati 30, nne zimekamilika za Ikengele, Bugabu,Isangijo na Bundilya zingine  17 majengo yamekamilika na zilibaki maboma yanajengwa. Hivyo nichagueni nitandelea kwenda kuchapa kazi hii kwa uadilifu na uwajibikaji wangu mnanifahamu vizuri.

Kiswaga pia amewaombea kura Madiwani wa CCM Velina Emmanuel Kata ya Isandula, Sambo Malaki kata ya Itumbili na Mashaka Mathias kata ya Magu mjini. Pia wamchague Rais Magufuli kwa kura nyingi na za heshima kwa kazi kubwa na nzito aliotendea Nchi yetu na Wilaya yetu.

‘Tumetekeleza kwa kishindo  Tunasonga mbele kwa pamoja’
‘TUNTUME HANGI KISWAGA ATOSHIJE’

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages