WANADIPLOMASIA wameisifu Tanzania kuwa ni nchi ambayo ni kisiwa cha amani, kutokana na kudhihirishwa na kutamalaki kwa hali ya amani na utulifu wakati huu wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, hali ambayo wamesema imechangiwa kwa kiasi kikubwa na wagombea wa nafasi mbalimbali za kisiasa hasa wa chama tawala (Chama Cha Mapinduzi) kufanya kampeni za kistaarab.
Sifa hizo zilizoambatana na pongezi kwa Watanzania zimetolewa leo kwa nyakati tofauti na Mabalozi wa Nchi mbalimbali wakiwemo wa Nchi za Kenya, Msumbiji, Marekani na wa Umoja wa Ulaya (EU), wakati walipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM , Lumumba Jijini Dar es Salaam, na kisha Katibu Mkuu na Mabalozi hao kuzungumza na Waandishi wa Habari.
Kila Balozi alielezea kufarijika ni kile wanachokiona kuwa wagombea wa nafasi mbalimbali nchini wamekuwa , wakitumia vyema majukwaa ya kampeni kwa kueleza ahadi watakazofanya wakichaguliwa kwa nafasi wanazoomba, badala ya kueneza chuki zinazohatarisha amani kama ilivyo katika baadhi ya mataifa mengine.
BALOZI WA KENYA
Balozi wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu, alisema kinachoendelea kushuhudiwa katika michakato na kampeni kwenye uchaguzi wa Tanzania mwaka huu ni kielelezo cha kudumishwa kwa amani iliyotokana na siasa safi na uongozi bora na kusema sasa ni wajibu wa Tanzania kuambukiza amani iliyonayo kwa mataifa mengine hususan ya Afrika Mashariki.
Balozi Kazungu, alisema ili kudumisha Demokrasia ni inabidi kuanza kwa kuimarisha vyama vya siasa, na kwa kutambua hilo, katika mazungumzo yao, amemuomba Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally, Oktoba 25, mwaka huu, Vijana wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha ODM, kuja nchini ili kujifunza namna Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) unavyoendesha Programu zake na katibu Mkuu huyo ameridhia.
“Hakuna nchi inayojua umuhimu wa amani katika Afrika Mashariki zaidi ya Tanzania na sisi tunatambua kuwa amani hiyo ni muhimu hata kwa Kenya ni vyema tuidumishe kwani ndio msingi wa maendeleo.
Faraja yetu ni kusikia siasa ya Tanzania imeghubikwa na sera za aina gani, wagombea watawafanyia nini wananchi baada ya kuchaguliwa, kama siasa haitakuwa marumbano tutafikia hatua kubwa,” alisema Balozi Kazungu na kuongeza;
“Tulipenda kuwa na ushirikiano na Chama Cha Mapinduzi, Oktoba 25 vijana wa chama cha ODM, watakuja kujifunza namna UVCCM inavyofanya kazi za kisiasa, tunashukuru tumekubaliwa hivyo vijana watakuja siku hiyo”. alisema kazungu huku akiipongeza Tanzania kwa kufanikiwa kuingia katika nchi zenye uchumi wa kati kabla ya muda uliotarajiwa na Benki ya Dunia wa mwaka 2025..
BALOZI WA MSUMBIJI
Naye Balozi wa Msumbiji Monica Mussa, alisema nchi yake inatambua kazi kubwa ya kudumisha amani inayofanywa na Tanzania hasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi wa mwaka huu ambao kwa mara nyingine tena unashirikisha vyama vingi.
Alisema amani iliyopo nchini imewafanya hata wananchi wa Msumbiji, kutembelea nchini bila kubughudhiwa na kushauri kuimarishwa kwa umoja na ushirikiano baina ya mataifa hayo, kama alivyotaka Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
"Tunafurahi na kutembea kifua mbele kwani sisi watu wa Msumbiji tunakuja Tanzania kama nyumbani, hatujioni kama tupo ugenini, na hii ni kwa sababu ya uhusiano na ushirikiano uliodumu kwa mda mrefu kati ya nchi zetu hizi mbili", alisema BaloziMonica.
BALOZI WA MAREKANI
Baada ya mazungumzo na Balozi wa Marekani Dk. Donald Wright, Dk. Bashiru alisema pamoja na mambo mengine balozi huyo pia ameipongeza Tanzania kwa kufanya kampeni zilizotamalaki usalama na amani na kushauri akisema, ili kuendelea kudumisha amani hiyo, ni muhimu kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki.
Dk. Bashiru, alisema katika mazungumzo yao alimhakikishia balozi huyo kudumishwa kwa amani katika michakato yote ya uchaguzi wa mwaka huu na kuongeza kuwa mambo mengine waliyozungumza na Balozi huyo ni kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani katika kuimarisha uchumi.
Alisema Balozi huyo alifafanua vipaumbele vya Marekani kwa Tanzania ni kuboresha mahusiano, kuboresha huduma za afya hususan kukabiliana na Kifua kikuu, Malaria, Ukimwi na mambo mengine ikiwemo kuboresha mahusiano juu ya uwekezaji ambapo akifafanua kuwa Tanzania ina maeneo mazuri ya uwekezaji.
Dk. Bashiru alisema Balozi huyo ameainisha kuwa maeneo mengine ya ushirikiano ni uhifadhi wa mazingira, wanyamapori na sekta ya utalii, kadhalika kuboresha uhusiano baina ya watu wa mataifa hayo katika masuala ya utamaduni na undugu.
MABALOZI WA EU
Akizungumza baada ya kikao na mabalozi wa Umoja wa Ulaya Dk. Bashiru, alisema mazungumzo yao yalihusu masuala ya uchaguzi na waliliombea mema taifa la Tanzania katika kufanikisha uchaguzi kwa Uhuru, haki na amani na kwamba mabalozi hao walieleza kuridhishwa kwao na kasi ya maendeleo inayopiga Tanzania chini ya Rais Dk. John Magufuli.
Dk. Bashiru alisema, mabalozi hao walikuja wanane akiwemo kiongozi wao ambaye ni Kamishna Mkuu wa Umoja wa Ulaya Balozi Manfredo Fenti, na kuwataja wengine katika ujumbe huo kuwa ni Anders Sjoberg wa Sweeden, Adrian Fitzgerald wa Ireland, Regme Hess wa Ujerumani, Jorean Verheul wa Uholanzi, Peter Van wa Ubelgiji, Kryett Buzalde wa Poland, Roberto Nengoni wa Italia na Mette Dissing wa Dernmark.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akiwa na Mabalozi wanane wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Ulaya (EU) wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, kabla ya kufanya nao mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam. Mabalozi hao ni kiongozi wao ambaye ni Kamishna Mkuu wa Umoja wa Ulaya Balozi Manfredo Fenti (aliyeketi kulia kwa Dk. Bashiru), na wengine katika ujumbe huo ni Mabalozi Anders Sjoberg wa Sweeden, Adrian Fitzgerald wa Ireland, Regme Hess wa Ujerumani, Jorean Verheul wa Uholanzi, Peter Van wa Ubelgiji, Kryett Buzalde wa Poland, Roberto Nengoni wa Italia na Mette Dissing wa Dernmark.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally (wa nne kulia) akiwa na Mabalozi kutoka Nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini,baada ya Mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo.
Katibu Mkuu wa CCM Dk, Bashiru Ally akimkaribisha Balozi wa Marekani hapa nchini Dk. Donald Wright alipofika Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya mazungumzo.👇
Katibu Mkuu wa CCM Dk, Bashiru Ally akimkaribisha Balozi wa Marekani hapa nchini Dk. Donald Wright alipofika Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa CCM Dk, Bashiru Ally akimkaribisha Balozi wa Marekani hapa nchini Dk. Donald Wright alipofika Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa CCM Dk, Bashiru Ally na Balozi wa Marekani hapa nchini Dk. Donald Wright wakifurahia jambo kabla ya mazungumzo yao alipofika Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa CCM Dk, Bashiru Ally akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini Dk. Donald Wright alipofika Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa CCM Dk, Bashiru Ally akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa Marekani hapa nchini Dk. Donald Wright katika Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa CCM Dk, Bashiru Ally akiwa na Balozi wa Marekani hapa nchini Dk. Donald Wright
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akizungumza na Waandishi wa habari baada ya mazungumzo yake na Balozi wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu (aliyevaa barakoa).
Balozi wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu akizungumza yaliyojiri baada ya mazungumzo yake na katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally (kushoto)
Balozi wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu na Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally baada ya kuzungumza na Waandishi wa habari.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akimsindikiza Balozi wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu baada ya mazungumzo yao.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akiagana na Balozi wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu baada ya mazungumzo yao
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akifurahi kwa tabasam wakati Balozi wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu akimwelekeza staili ya kuagana kwa ajili ya kujikinga na Corona, wakati wakiagana baada ya mazungumzo yao. Nchi ya Kenya bado inakabiliwa na virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa huo wakati Tanzania hakuna
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akizidi kuelekezwa na Balozi wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu
"Tuagane kwa kufanya hivi......", akisisitiza Balozi Kazungu
Kisha wakaagana
katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akipunga mkono kumuaga Balozi kazungu wakati gari alilomo likiondoka, na muda si mrefu akawasili Balozi wa msumbiji hapa nchini Monica Mussa👇
Balozi Monica akishuka kutoka kwenye gari lake
Balozi Monica akipiga shoto kulia kumwendea katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally aliyekuwa akimsubiri kwa hamu
Wakasalimiana kwa bashasha
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashir Ally akiongozana na mgeni wake Balozi wa Msumbiji Monica Mussa kwenda ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo
Katibu Mkuu wa CCM Dk. bashiru Ally akimsubiri Balozi Monica asaini kitabu cha wageni ili mazungumzo yaanze.
Kisha akapiga naye picha ya ukumbusho.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akiagana na Balozi wa Msumbiji hapa nchini Monisa Mussa baada ya mazungumzo yao.
Byeeee: Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akimuaga kwa heshima zote Balozi wa Monica wakati gari likianza kuomndoka. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO- CCM Blog.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇