Viongozi mbalimbali wameanza kupiga kura katika uchaguzi unaoendelea Tanzania miongoni mwao akiwa Hussein Mwinyi anayegombea urais Zanzibar.
''Nawapongeza Wanzanzibar wote ambao wametumia haki yao ya kupiga kura na niwaombe ambao hawajafika waendelee kujitokeza kupiga kura na hatimaye zoezi liishe kwa amani'' Bwana Mwinyi amesema.
Raia nchini Tanzania wameanza kupiga kura kuchagua viongozi wao watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa kuanzia saa moja majira ya asubuhi tayari kwa zoezi hilo.
Mwanahabari wa BBC Eagan Salla alitembelea ofisi ya mtendaji wa mtaa wa Kunduchi Mtongani eneo ambalo makarani na wasimamizi wa vituo vya kupigia kura walikuwa wanachukua vifaa, vituturi, karatasi za kupigia kura pamoja na masanduku ya kuwekea kura baada ya kura kupigwa.
Hali imekuwa ni harakati za makarani wakiingia na kutoka eneo hilo kuelekea maeneo yao husika wanayosimamia zoezi la uchaguzi.
Pia katika vituo vya kupigia kura muda wa mapema wakati mwanahabari Eagan Sallah anatembelea watu walikuwa sio wachache wala wengi sana wanaowasili kila mmoja kwa wakati wake wakiendelea kuhakikisha taarifa zao kwenye makaratasi ambayo yamebandikwa kwenye kuta.
Your Ad Spot
Oct 28, 2020
DK HUSSEIN MWINYI APIGA KURA ZANZIBAR
Tags
featured#
siasa#
Zanzibar#
Share This
About Richard Mwaikenda
Zanzibar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇