LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 9, 2020

ZAINABU VULU AWATAKA WANANCHI MKURANGA KWENDA WOTE KUIPIGIA KURA CCM OKTOBA 28, 2020

 Na Scolastica Msewa, Mkuranga.

Mgombea ubunge viti Maalumu wanawake Zainabu Matitu Vulu amewataka wanaCCM kuhakikisha siku ya kupiga kura kila mmoja anatoka akiwa ameambataka na wote wa nyumbani kwake kuelekea kwenye kituo cha kupiga kura ili kuhakikisha wananchi wa Mkuranga wanakwenda wote kupiga kura kwa CCM.


Ameyasema hayo mjini Mkuranga katika mkutano wa ndani wa Uzinduzi wa Kampeni za jimbo hilo katika viwanja vya CCM wilaya ya Mkuranga ambapo kabla ya mkutano wa hadhara alipata nafasi ya kuongea kwanza na walioomba nafasi ya kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge na udiwani pamoja na Wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya.


Vulu kila mwana CCM siku ya kupiga kura ya uchaguzia mkuu ahakikishe anaatoka nyumbani kwake akiwa na wanafamilia wote kwenda nao kwenye kituo cha kupiga kura ili kuhakikisha wote waliojiandikisha wanatumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.


Aidha Vulu akiwataka wanaCCM na wananchi kwa ujumla kuangalia maslahi ya taifa katika upigaji kura zao kwa Chama kilichoonyesha mwelekeo wa maendeleo kwa taifa siku ya octoba 28 mwaka huu badala ya kupiga kura kwa chama kisichona mwelekeo.


Mgombea huyo wa ubunge viti maalumu mkoa wa Pwani awali alianza kwa kuwashukuru akinamama kwa kumpigia kura katika mkutano mkuu wa kura za maoni.


Aidha Vulu amewataka kumchagua kwa kura nyingi za kishindo Mgombea Urais wa CCM Dr. John Pombe Magufuli ili aweze kuendelea kuongoza nchini.


Katika mkutano huo amemnadi Mgombea wa ubunge Abadallah Ulega na amewanadi wagombea udiwani 25 wa kata za wilaya Mkuranga.

Mgombea ubunge viti Maalumu wanawake Zainabu Matitu Vulu  akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Mkuranga.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages