LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 17, 2020

WENYE NYAVU HALALI RUHUSA KUVUA SAMAKI MUDA WOWOTE- DC MSAFIRI

 

IMG-20200916-WA0134

Mkuu wilaya ya Kigamboni Mhe.Sarah Msafiri leo amefanya kikao na wavuvi wote wa ferry katika kata ya kigamboni ambapo ameongozana na mgombea ubunge jimbo la kigamboni Dkt.Faustine Ndugulile pamoja na mgombea udiwani kata ya kigamboni Ndg.Dotto Msawa.


Mgombea udiwani Ndugu Dotto Msawa amewaeleza wavuvi kuwa serikali ipo kwa ajili ya kuwatetea wananchi wake wote kwa maana ndani ya ilani ya CCM huelekeza hivo na nia ya Mhe.Rais Magufili ni kuhakikisha kila mwananchi anafaya kazi yake pasipo kusumbuliwa hivyo leo hii ufafanuzi utatolewa na zaidi yeye kama mwakilishi wa wananchi ngazi ya kata  yupo kusikiliza pamoja na mwakilishi mwenzake ngazi ya jimbo Dkt.Ndugulile.


Katika kikao hichi wavuvi walikuwa na ombi la kuvua mchana kuweza kupata ridhiki na kupata nguvu ya kuendelea kushiriki mambo mengine kijamii.


Mgombea ubunge Dkt.Ndugulile amewaeleza wavuvi kuwa matarajio yake kwa kushirikiana na viongozi wenzake ni kuboresha mifumo ya uvuvi na hali ya maisha ya wavuvi "Najua mnafanya kazi kwa wakati mgumu niwashawishi mjiunge katika vikundi mtapewa elimu na Afisa maendeleo yupo,tutambe kuwa 10% ya mikopo Halmashauri hata  nyinyi mnapatiwa" Alisema Dkt.Ndugulile.


Aidha katika maelezo yake Mkuu wa wilaya Mhe.Sarah amesema "Jukumu langu ni kulinda maisha ya wananchi kiusalama na kusimami shughuli zote wilayani,nimshukuru mteule mgombea ubunge Dkt.Ndugulile alilipeleka hili kwa Mhe.Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ile siku ya mkutano mjimwema na sasa nimeletewa goli lipo wazi ni kufanga tuu,ninachotaka kusema ninachojua kuna nyavu ambazo zinaruhusiwa kwa mujibu wa sheria,mwenye nyavu hizo avue muda wowote iwe asubuhi,mchana au usiku..fanyeni shughuli zenu kupata mapato yenu kujiinua kiuchumi"


Aidha Mhe.Sarah amesema kuwa mara baada ya kikao atamuandikia OCD barua na polisi marine kutokukamata wavuvi na kuongeza kuwa wasiokuwa na leseni ya uvuvi amewapa wiki mbili kuvua ilikupata fedha ya kupata leseni baada ya wiki mbili bila leseni watakamatwa.

IMG-20200916-WA0135

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages