Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na tukio la ujambazi wa kutumia silaha lililosababisha kujeruhiwa kwa wananchi sita katika Kijiji cha Kalela Wilayani Kasulu mkoani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, James Manyama ameeleza kuwa katika tukio hilo pia silaha moja aina ya AK47, magazine moja pamoja na risasi 45 zilikamatwa kutoka kwa majambazi hao.
Manyama ameeleza kuwa kati ya majambazi watatu ambao walivamia soko katika Kijiji hicho cha Kalela wawili kati yao waliuawa na wananchi wakishirikiana na Polisi huku mmoja akikimbia ambapo wananchi wa tatu wanashikliliwa kwa uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇