LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 2, 2020

TOUFIQ: WANAWAKE TUTAWASHAWISHI WAUME ZETU WOTE WAMPIGIE DK MAGUFULI KURA NYINGI APATE USHINDI WA KISHINDO

 Mgombea Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma, Fatuma Toufiq  (kushoto) akijinadi huku akiahidi yeye na Wanawake wa Mkoa wa Dodoma watafanya kampeni kwa kuwashawishi waume zao ili ifikapo Oktoba 28, mwaka huu wanampigia Dk. John  Magufuli kura zote apate ushindi wa kishindo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa  CCM, Dk. Bashiru Ali,, Rais Magufuli, Makamu Mwenyekiti, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Tukio hilo lilitokea baada ya Toufiq kukaribishwa jukwaa kuu kujinadi yeye pamoja na wagombea wengine wa CCM,  ambapo kwa kuona wanawake ni jeshi kubwa na lenye ushawishi mkubwa katika jamii, alisababisha viongozi waliokuwa   jukwaa kuu kuangua vicheko na hadhara iliyofurika uwanjani hapo  pia kucheka, hasa baada ya kusema yeye na wanawake wa mkoa wa Dodoma watahakikisha wanawashawishi waume zao wampigie kura za urais Dk. Magufuli.

Viongozi hao wakiongozwa na Mgombea Urais wa Tanzania, Dk. Magufuli, Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan na Mgombea Urais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi pamoja na marais wastaafu, Ali Hssan Mwinyi na Dk. Jakaya Kikwete walifurahishwa na mtindo huo wa kampeni ambapo licha ya kuonekana kuwa na furaha kwa kicheko lakini pia walimpigia makofi Toufiq huku wakimwangalia.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za CCM, katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Agosti 29, 2020 uliofurika wananchi, Toufiq hakuishia hapo, alisema kuwa wanawake wataendeleza kampeni yao kwa kuwashawishi pia  watoto wao, vijana wao, marafiki na jamaa zao pamoja na wananchi  kwa ujumla wampigie Dk. Magufuli kura nyingi za ndiyo.

Baada ya kumaliza kunadi, Toufiq  ambaye pia alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni kabla ya kugombea nafasi ya ubunge, alikabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali, Kitabu cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, na kuelekea jukwaa lingine walilopangiwa kukaa.

 

Fatuma Toufiq akiingia jukwaani kujinadi yeye pamoja na wagombea wengine wa CCM na hasa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli (wa pili kulia).  Viongozi wanaomwangalia kutoka kulia ni; Katibu Mkuu wa  CCM, Dk. Bashiru Ali, Makamu Mwenyekiti, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk.  Hussein Ali Mwinyi. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Toufiq ambaye aliongoza kura za maoni za ubunge Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa CCM  (UWT) Mkoa wa Dodoma, akiendelea kunadi ili wananchi wawachague wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages