LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 12, 2020

TATHMINI: CCM IMESIMAMA KWENYE HOJA, WENGINE VIOJA

MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA...

Msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli ukiwa Katoro, mkoani Geita wakati wa kampeni za chama hicho. 

Na Mwamba wa Kaskazini

Tunaweza kwa viashiria vyote  kukubaliana kuwa awamu flani ya awali ya kampeni za uchaguzi kwa ajili ya Urais wa Jamhuri ya Muungano imekamilika na vyama na wagombea vinajipanga kuendelea tena.

Hii ni baada ya kuoneakana wazi kuwa wagombea karibu wote wakuu wamepita mikoa kadhaa, kubadili baadhi ya mbinu ikiwemo wengine kutokomea nje ya nchi lakini kubwa ni kuanza kwa kampeni za Urais wa Zanzibar wikiendi hii.

Kwa tathmnini fupi niliyoiona ni kama ifuatavyo:

1. CCM: Mgombea wake ameishi ahadi yake, amepiga kampeni ya kiwango cha juu, ya kistaarabu, amepita mijini na vijijini kwa gari na kwa barabara, ametetea utendaji wake, ameeleza mafaniko yake, ameeleza magumu aliyokutana nayo na amejenga hoja kwa nini apewe miaka mitano tena akakwamue yaliyobaki.

Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea wa CCM, anakipawa cha kuongea, kushawishi na kujenga hoja, ndicho ninachoweza kusema.

Amesadifu kile wachambuzi wa ubora wa wagombea wanachokisema katika "*Say It Like Obama; The Power of Speaking With A Purpose and Vision*."

Katika fasihi hiyo mwandishi Shel Leanne, anasema ubora au udhaifu wa kiongozi unaweza kuonekana vyema katika hotuba zake anapoweka na kuainisha mtazamo wake, anapojenga hoja zake na anapoainisha mikakati yake.

Katika siku takribani 10 alizochapa mwendo katika kampeni yake ya #MitanoTena Rais Magufuli amethibitisha si tu ana kipawa cha kuongea with a "purpose and vision" bali ameonesha anajambo lake; kukamilisha mageuzi aliyoyaanzisha ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Na ndio maana, anapojitokeza mbele ya wanahabari hata Msemaji wa CCM, ndugu Polepole anasema kwa furaha na kujiamini kuwa pangefanyika uchaguzi leo, wangeshinda kwa zaidi ya asilimia 85.

2. ACT-Wazalendo: Kuna mwanafalsafa mmoja wa kale aliwahi kusema vitendo huongea zaidi ya maneno (actions speak louder than words).

Ukiangalia kauli alizokuwa akizitoa kiongozi wa Chama hiki kuwa wao ndio mbadala na wanasubiri kampeni waoneshe uwezo wa Chama hicho katika siasa, unaweza leo unapokitathmini chama hiki hata ukakisahau kama kipo katika kampeni au la.

Kimedorora, kimeshindwa kufanya siasa, kimeshindwa kujitangaza wala kunadi sera zake na zaidi mgombea wake kaweka rekodi ya dunia kwa mgombea Urais kwanza kutumia zaidi ya wiki akiwa mkoani kwao kama mgombea ubunge hivi na kisha kuacha kampeni na kukimbilia nchi za nje!

Kiongozi wake Mkuu wa Chama kabaki maneno maneno tu mitandaoni huku akiweka rekodi ya kupanda ndege ya Bombardier Q400 jana kutoka Dar kwenda kwao Kigoma, huku akiwa alizibeza ndege hizo kuwa ni maendeleo ya vitu na si watu na kuhoji usalama wake akidai zilikuwa si mpya bali za zamani zilizotolewa huko Vietnam!!

Kwa kifupi ni Cha chenye maneno maneno mengi lakini katika siasa kimeshindwa na ni dhahiri kimekwama na zipo tetesi kuwa mgombea wao wa URais Ndugu Membe, kama atarudi, basi huenda akajiunga na Chadema. Kwa kifupi wanaonekana wako hoi kisiasa, hoi hata kifedha.

3. CHADEMA: Kama kuna mgombea ambaye anatanzika kifalsafa, kisiasa na kiuchaguzi ni Tundu Lissu. Ni mwanasiasa ambaye ana hulka mbili.

Mosi, kuona kwamba kila kilichofanyika katika nchi yake ni kibaya lakini hicho hicho kikifanyika kwa wazungu ni safi. Ashaponda ndege, anaponda barabara zinazojengwa, anaponda viwanda, anaponda madaraja, anawaponda viongozi, amewaponda majaji kuwa hawajui Kiingereza, amewaponda watumishi wa umma, amewaponda wanahabari.

Pili, ni mwanasiasa ambaye unamuona kabisa kuwa amebadilika kutoka yule mpinga ubeberu na sasa amekuwa "compromised" hadi kuwa wakala wa mabeberu.

Na anasema wazi katika kampeni zake kuwa eti wazungu wanafuatilia, eti akionewa kuna wazungu watamsaidia!!!Ni kiongozi, huenda wa kwanza Afrika, anayesema wazi na anayetamka wazi kuwa eti atawaita wazungu kuingilia kati masuala ya nchi yake.

Ni mwanaharakati mropokaji asiyetoa matumaini yoyote katika maisha ya Watanzania.

Anatanzika asimamie hoja gani? Hawezi kuahidi barabara kwa sababu ameziponda kuwa si maendeleo ya watu, hawezi kuahidi viwanda, ameviponda kuwa si maendeleo ya watu, hawezi kuahidi kuendeleza miradi mikubwa na yenye impact kwa wananchi kama SGR, Mradi wa Umeme Rufiji kwa sababu vyote ameviponda.

Lakini aliponda ndege yeye naye sasa anatumia ndege kufanya kampeni tena akiruka na kupishana na wananchi wengi na kutua kwenye vituo mahsusi vya mijini ambako kazi kubwa ya kuzoa watu kwa malori inakuwa imefanyika ili walau kumuondolea aibu ya kukosa watu.

Ukitaka kujua jamaa ametanzika angalia hata Msemaji wa Chama chake mara ambazo ametoa taarifa za Chama hicho mpaka sasa, tofauti na kule CCM yameelezwa masuala na hoja na confidence waliyonayo, huku ni mwendelezo wa malalamiko tu; tumenyimwa kibali cha kurusha ndege (wakati wamekiuka masharti ya usafiri wa anga), tunaonewa, tutavunja baadhi ya taasisi za umma n.k.

Yani ni Chama cha malalamiko na si kutangaza Ilani yao.

Vyama vingine vya kisiasa kama Chaumma na NCCR Mageuzi kimsingi vipo na vinafanya kampeni lakini bado havijajipambanua sana nini hasa hoja zao za masingi, hata hivyo vinasaidia kuhubiri amani na upendo kwa Watanzania.

Niite Mwamba (mara 3) wa Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages