LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 11, 2020

RAIS MAGUFULI KUTINGA BUKOBA MKOANI KAGERA SIKU YA JUMANNE YA WIKI IJAYO

 

Mgombea Urais wa CCM, Rais Dk. John Magufuli


Na Lydia Lugakila, Bukoba

Mgombea Uras kwa tiketi ya CCM, Rais Dk. John Magufuli  anatarajiwa kuwasili mkoani Kagera siku ya Jumanne, Septemba 15, 2020 kuendelea na awamu ya pili ya Kampeni zake za kusaka kura kwa wananchi ili kuibuka na ushindi wa kishindo kwa kura nyingi katika uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwishoni mwezi ujao.


Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Kagera Hamimu Mahamood amewaambia waandishi wa habari leo kwamba baada ya kuwasili Mgombea huyo wa Urais Dk. Magufuli atakutana na Wananchi katika maeneo mbali mbali na baadaye kuhutubia mkutano wa Kampeni katika Viwanja vya Gymkhana, vilivyopo katika Manispaa ya Bukoba.


Amesema Dk. Magufuli mbali na kuwaomba wananchi kuichagua CCM atazungumzia jinsi Serikali ya awamu ya tano anayoiongoza ilivyofanikiwa katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya 2015-2020 na namna gani CCM imejipanga kukamilisha au kufanya miradi mipya iliyoianisha katika Ilani yake ya Uchaguzi wa mwaka huu wa 2020.


Mahamood amesema, kesho yake, Septemba 16, 2020 ataondoka Bukoba mjini na kwenda Wila ya Muleba kuendelea na ziara yake ya kampeni katika mkoa huo wa Kagera.


Mwenezi huyo amewataka wana CCM na wananchi kwa jumla kujitopkeza kwa wingi ili kuweza kusikiliza wenyewe Mgombea wa Urais wa CCM Dk Magufuli atakayozungumza badala ya kusubiri kusimuliwa na hatimaye kuambiwa uwongo.

5 comments:

  1. Siku zote Huku hatuna wasi wasi na dokt Jpm ni suala la muda tu

    ReplyDelete
  2. Huyu ni jembe mashine mtu makini hayumbishwi na hateteleshwi na yoyote Tuchape kazi..

    ReplyDelete
  3. Sisi Vijana tuna muunga mkono Mh Rais katika michakato huu uliopo mbele yetu. Tutahakikisha kuwa anashinda kwa Kishindo ccm oyeeeeee!

    ReplyDelete
  4. Rais Wetu Kiongozi Mkuu Imara Mungu Amlinde JPM AFIKE salama akawahudumi

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages