Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania Fortunatus Muslim, amefika katika stendi kuu ya mabasi mkoani Arusha nakufanya ukaguzi wa magari ambapo ametoa onyo kwa madereva wanaokimbizana barabarani kwa lengo lakupewa fedha pale wanapowahi kufika stend.
“kuna baadhi ya madereva wanabet,nasikia kuna kikundi cha watu wanawapa fedha wale wanaokuwa wa kwanza kufika pale”-Kamana Muslim
Kwa upande wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha Solomon Mwangamilo ,ametoa tahadhari kwa madereva wa makampuni ya magari yaliyotajwa kuhusika na mwendo mkali barabarani.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇