Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu (RMO) wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Best Magoma mashuka 180 kwa ajili ya hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
*****************************
Benki ya NMB, imetoa msaada wa madawati 50, mashuka 180 na ndoo za kunawia vyote vikiwa na thamani ya zaidi Sh11 milioni. Msaada huo ulikabidhiwa kwa uongozi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma na madawati 50 kwa shule ya msingi Mnadani ya jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi misaada hiyo, Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi alisema kutolewa kwa msaada huo ni sehemu ya utaratibu waliojiwekea katika kurudisha faida waliyopata kwa jamii.
Mlozi alisema kwa kipindi cha mwaka huu, mkoa wa Dodoma ndiyo umeongoza kwa kupata misaada mingi kutoka NMB kwa kuwa hadi sasa wameshatao msaada wa vitu mbalimbali vyeye thamani ya shilingi milioni 120.
Akieleza kuhusu misaada hiyo, Mlozi alisema kutoka na jiji la Dodoma kuwa na ongezeko kubwa la watu kulikotokana na kukuwa kwa mji, mashuka hayo 180, yatasaidia kupunguza changamoto zilizo katika hospitali hiyo ikiwemo wodi ya akinamama na watoto. Kuhusu madawati alisema wameichagua shule ya msingi Mnadani baada ya kupata maombi kuwa shule hiyo licha ya kuwa katikati ya mji lakini ilikuwa na upungufu mkubwa wa madawati.
Kuhusu ndoo 50 zilizotolewa alisema zitatumika kunawia mikono ikiwa ni sehemu ya kuendeleza usafi ili kukabilina na magonjwa mbalimbali ya mlipuko ikiwemo maambukizi ya virusi vya corona hasa kwenye mikusanyiko ya watu.
Akipokea msaada huo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Best Magoma alipongeza Benki ya NMB kwa msaada huo na kusema kitendo hicho kinaonyesha ni jinsi gani Benki hiyo siku zote inaendelea kuudhirihishia umma ni jinsi gani wapo karibu na jamii katika kusaidaia Sekta za Afya na Elimu nchini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇