Benki ya NMB
inatarajia kukusanya zaidi ya Sh. milioni 100 kwa ajili ya matibabu ya watoto
wenye saratani katika mbio za NMB Bima
Marathon zilizopangwa kufanyika Septemba 12 jijini Dar es Salaam.
Fedha hizo
zinatarajia kupatikana kupitia kwenye ada ya ushiriki wa mashindano hayo kwa
upande wa Kilometa 5 ambazo zitashirikisha wadau mbalimbali watakaojitokeza
kushiriki katika mbio hizo zilizopangwa kuanzia jengo la Mlimani City.
Afisa Mkuu wa
Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB - Filbert Mponzi alisema kuwa
wanatarajia kushirikisha jumla ya wanariadha 3,000 katika mbio hizo
ambazo zimeandaliwa na kampuni ya The Africa Digital Banking Summit
inayoongozwa na Baraka Mtavangu.
Add caption |
Afisa Mkuu wa Binafsi na Biashara wa Benki ya
NMB, Filbert Mponzi akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
jijini Dar es Salaam kuhusiana na Mbio za NMB Bima Marathon zitakazofanyika
Jumamosi ijayo. Kushoto ni Mwakilishi wa waandaaji wa mbio hizo, Baraka
Mtavangu na Mwakilishi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Rehema
Laiti.
Mponzi
alisema kuwa, viingilio vyote vya mbio za kilometa 5 vitapelekwa kwenye
hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu ya watoto hao. Alisema kuwa, mbio
za kilometa 10 na 21 zitatumika zaidi kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na
umuhimu wa bima.
“Tunajisikia
fahari kudhamini mashindano haya kwa ajili ya kusaidia jamii. Tunaomba wadau
washiriki ili kufanikisha lengo au kuzidi lengo hilo. Naomba pia nitoe rai kwa
jamii nzima aidha kushiriki mbio hizi au kuwasajili ndugu na marafiki ili
tuweze kuwagusa watoto wengi zaidi wenye saratani kupata matibabu hospitali ya
Muhimbili,” alisema Mponzi.
Hizi ndizo jezi zitakazotumika
Timu ya NMB
ikiwa tayari kwaajili ya Mbio za NMB Bima Marathon.
Kwa upande
wake Baraka Mtavangu ambaye ni Mratibu wa NMB Bima Marathon alisema sehemu za
kujisajili ni Mlimani city karibu na KFC pamoja na hospitali ya muhimbili. Wale
wote ambao tayari wameshajisajili wanaweza kupata jezi zao hapo hapo Mlimani city
karibu na KFC.
Mbali ya
Benki ya NMB, wadhamini wengine ni kampuni za Bima za Sanlam, Strategies,
Reliance na UAP. Benki hiyo kama mdhamini mkuu imetoa Shilingi
milioni 35 kwa ajili ya udhamini wa mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇