LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 4, 2020

NAPE, JAMES WATEMA CHECHE UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM JIMBO LA ILEMELA

 

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe Kamati kuu ya CCM Komred Kheri James, akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela kupitia CCM, Angelina Mabula wakati wa   uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi ktk Jimbo hilo mkoani Mwanza.

katibu Mwenezi wa zamani wa CCM, ambaye amepita bila kupingwa kugombea ubunge jimbo la mtama,Lindi, akimwaga sera alipokuwa akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula wakati wa uzinduzi wa kampeni katika jimbo hilo. 

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe Kamati kuu ya CCM Komred Kheri James (MCC) amewaongoza wanachama na wananchi katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi ktk Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.

Katika uzinduzi huo,Komred Kheri James amemnadi mgombea wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula,pamoja na madiwani wa Kata zote 19 za jimbo hilo.

Komred Kheri James(MCC)ameitumia fursa hiyo kueleza ubora wa Ilani ya uchaguzi ya CCM pamoja na umahiri wa wagombea wa chama Cha Mapinduzi wa ngazi zote,na amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 28/10/2020 kupiga kura kwa wingi ili chama cha mapinduzi kipate nafasi ya kuendeleza maegeuzi makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo kwa maslahi ya Taifa letu na watu wake wote.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi wa mkoa wa CCM,wilaya,kata,matawi,mashina,wananchi,pamoja na wagombea wa majimbo jirani wakiongozwa na Mh.Mbunge mteule wa jimbo la Mtama Komred Nape Moses Mnauye.

#Tukutane kazini..



 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages