LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 11, 2020

MUSEVENI: 'MKAKATI NINAOUTUMIA KUWASHAWISHI VIJANA'


Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amekuwa akizungumzia mkakati anaotumia kuwavutia vijana katika mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na wale ambao "wananitukana ,wakisema, wewe ni mjinga sana".

Alisema mkakati wake ni kufanya mijadala thabiti ili kuwashawishi wakosoaji wake.

"Sihitaji kulumbana na hawa watoto ili kuwashawishi, nikituma ujumbe kuwajibu kumi waliokuwa wakinishambulia, sita pekee wanabakia na wane wananijibu wakisema mzee ametoa hoja nzuri."

Bwana Museveni ameongoza Uganda tangu 1986 na atagombea urais kwa muhula wa sita katika uchaguzi mkuu ujao.

Miongoni mwa wale wanaopanga kumpinga katika kinyang’anyiro hicho ni msanii aliyegeuka mwanasiasa Bobi Wine, 38, ambaye ni maarufu kwa vijana.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages