Na Scolastica Msewa, Kibiti
Mgombea Ubunge Jimbo la Kibiti mkoani Pwani Twaha Mpembenwe ameahidi kushughulikia kupandisha hadhi barabara ya Ikwiriri Muyuyu hadi Mchukwi iwapo atashinda ubunge ili itoke kuhudumiwa na Tarura Hadi kuhudumiwa na Tanroads mkoa kwani inaunganisha wilaya mbili na gharama za matengenezo ni kubwa na halmashauri haziwezi.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Mtunda kwenye vijiji vya Muyuyu na Mtunda Mpembenwe amesema barabara hiyo inaunganisha wilaya ya Kibiti na wilaya ya Rufiji matengenezo yake yanahitaji gharama kubwa ili iweze kupitika majira zote.
Amesema kipindi cha Mvua nyingi vijiji vya muyuyu na Mtunda vinakuwa kama visiwa kwa kukosa mawasiliano ya barabara huwabidi wananchi wake kusafiri kwa mitumbwi jambo ambalo ni hatari kwasababu ya wanyama wakali kama mamba na maji nayo huwa ni makali jambo ambalo ni hatari kwa wananchi hao.
Aidha Mpembenwe ameahidi kushughulikia ujenzi wa daraja la Ruohi katika Mto Ruohi ambalo ndio linaweka mpaka kati ya wilaya ya Rufiji na wilaya ya Kibiti.
Amesema barabara hiyo yenye urefu wa kilo mita 48 ni kiunganishi muhimu kwa wakazi wa kata za Mtunda na Ikwiriri huwa ni kero kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇