Makoa akitoa ahadi kwamba akichaguliwa atafuatilia kero ya maji na kuitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Wagombea Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma wakijitambulisha na kumuombea kura Makoa na Dk. Magufuli pamoja na madiwani wa CCM. Kutoka kushoto ni Halima Okash na kulia ni Mariam Ditipile. Katikati ni Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga.
Na Mwandishi Wetu, Kondoa.
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kondoa Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ally Makoa amesema endapo akichaguliwa, ameahidi kwanza kulitafutia ufumbuzi tatizo kubwa la maji jimboni humo.
Amesema kuwa kama Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 inavyoeleza kwa Kondoa Mjini, atafuatilia ujenzi wa matanki makubwa ya kuhifadhi maji na kuboresha miundombinu iliyojengwa miaka ya 70 wakati huo idadi ya wakaazi ikiwa ndogo.
Mgombea huyo, ameahidi pia kufuatilia usambazaji wa umeme vijijini ambapo atahakikisha unawafikia wananchi.
Pia, ameahidi kushughulikia uboreshaji wa miundombinu ya barabara vijijini na kujenga Daraja la Mto Munguri linalowatesa wananchi wakati wa masika.
Amesema yote hayo yatafanikiwa iwapo tu wananchi watawapigia kura wagombea wa CCM wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇