LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 10, 2020

MGALU AMSHUKURU JPM KWA KUUPATIA MKOA WA PWANI SH. BILIONI 138 ZA KUSAMBAZA UMEME HADI VIJIJINI

 Na Scolastica Msewa, Rufiji.

Mgombea wa Ubunge viti maalumu mkoa wa Pwani na Naibu waziri wa Nishati Mheshimiwa Subira Mgalu amemshukuru Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi kwa niaba ya wana CCM na Wananchi wa mkoa wa Pwani kwa kuupatia mkoa huo zaidi ya sh. Bilioni 138 kwa ajili ya kusambaza umeme hadi vijijini.


Amesema hayo kwenye mkutano wa kampeni huko Ikwiriri rufiji mkoani Pwani pia amemshukuru Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu Hassani kwa namna ambavyo wamewezesha mkoa wa pwani kwa kuupatia shilingi bilioni 138 kwenye miradi ya umeme.


Amesema serikali ya awamu ya tano wakati inaingia madarakani ni vijiji 79 tu kati ya vijiji 421 vya mkoa mzima wa Pwani ndio nilikuwa na umeme katika mkoa huo wa Pwani sawa na asilimia 18 lakini kazi ya miaka 5 imewezesha vijiji vipya 268 kuwa na umeme sawa na asilimia 82 ya mkoa mzima.


Mheshimiwa Mgalu amesema Mgombea Urais Dr. John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu Hassani ni Majemadali wa mkoa huo wa Pwani kwa kuifanya hata nchi kuwa kwenye ramani ya kuwa ya kwanza kusambaza umeme hadi vijijini kuliko nchi zote barani Afrika.


Akizungumzia Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere katika mto Rufiji Mheshimiwa Subira amesema mabwawa yaliyokuwepo hayana uwezo wakuzalisha umeme kwa kiwango kikubwa Bwawa hilo kwani linatarajia kuzalisha zaidi ya megawatt 2115 na kuiweka nchi katika nafasi ya kwanza katika afrika mashariki kwani umeme huo utawezesha katika kila sekta.


“Kujenga Bwawa hilo kwa usubutu wa Mgombea wa Urais wa CCM ni kubwa na la aina yake mabwawa tuliyokuwa nayo ni kidatu huzalisha megawatt 204, Mtela inazalisha mega watt 80 , kihansi megawatt 180, nyumba ya mungu megawatt 97 na miradi mingine inazalisha megawatt 97 , kidatu kiasi hicho hakifanani na kiasi kitakachozalishwa kwenye bwawa la mwalimu nyerere” alisema Subira. 


“Nawaomba wana Pwani kwa tunu hii iliyofanya nchi yetu kuingia kwenye ramani ya ulimwengu hatuna sababu ya kufanya majaribio bali tuchague kazi za maendeleo ili kazi iendelee” alisema  Subira.


Amewataka wananchi wa mkoa wa Pwani wawapigie kura za kishindo  Mgombea Urais Dr. John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu Hassani ikiwa ni pamoja na wagombea wote wa CCM ili kufikia asilimia zaidi ya 90 ya kura zote ili wawawezeshe Wagombea wote wanne Viti maalumu washinde pia.

Subira Mgalu akizungumza kwenye mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages