LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 9, 2020

MAVUNDE AZIDI KUWAKOSHA WANANCHI KWA KUTOA AHADI ZENYE MASHIKO

Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akitoa ahadi lukuki katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Ntyuka, jimboni humo.
Mavunde (kushoto) akimnadi kwa wananchi mgombea Udiwani Kata ya Ntyuka, Yona Mambala wakati wa mkutano wa kampeni katika kata hiyo.

Wanachama, wapenzi wa CCM na wananchi kwa ujumla wakishangilia wakati Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Mavunde akiomba kura na kutoa ahadi za kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo endapo watampigia kura na kushinda katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Na Na Richard Mwaikenda, Dodoma.

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde endapo akichaguliwa, ameahidi kutatua mgogoro wa ardhi Kanda ya Kijani,  kusambaza maji Kata Mtyuka na kusambaza nishati ya umeme maeneo yaliyosalia jimboni humo.


Amesema ili aweze kutekeleze kiurahisi ahadi hizo na nyinginezo, aliwaomba wananchi kumpigia kura nyingi yeye, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli na madiwani wote 41 wa CCM, katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.


Mavunde ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye ulemavu, ametoa ahadi hizo wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Mtyuka, ambapo pia ameahidi ukarabati wa miundombinu ya barabara za ndani, kuboresha michezo na sanaa.


Pia, wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge uliofanyika hivi karibuni katika Kata ya Chang'ombe, kuwa kutumia mfuko wake binafsi, aliahidi kujenga visima vya maji, kusambaza kompyuta katika shule zote za msingi na sekondari jimboni humo.


Mgombea huyo kijana mwenye mvuto kwa wananchi na mchapakazi hodari, ametoa ahadi nyingine ya kujenga shule mpya ya msingi katika Mtaa wa Bwawani hivyo kuongeza wigo wa watoto wengi kujiunga na elimu ya msingi katika eneo hilo.


Muda wote ambao Mavunde alipokuwa anatoa ahadi, vilikuwa vinaibuka vifijo na vigelele kutoka kwa wananchi waliofurika kwenye mkutano huo wa kampeni. Alimnadi kwa wananchi mgombea udiwani wa Kata hiyo ya Mtyuka, Yona Mambala.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages