LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 9, 2020

MABULA AAHIDI MAENDELEO JIMBO LA ILEMELA, MWANZA



  

***********************************

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilemela kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt Angeline Mabula amesema kuwa ataendelea kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Ilemela kwa haki, usawa na uadirifu mkubwa kuhakikisha wananchi hao wanapata maendeleo.

Dkt Angeline Mabula ameyasema hayo wakati akihutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Masemele kata ya Shibula ambapo amewataka wananchi hao kuchagua viongozi wanaoweza kuwatumikia na kuwaletea maendeleo badala ya kujaribu watu wasiokuwa na maono ya kutumikia watu Zaidi ya kujinufaisha hao binafsi.

 Amebainisha miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa ndani ya jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitano ya utawala wake na wa Rais Mhe Dkt John Magufuli ambapo hospitali ya wilaya imejengwa, shule mpya tatu za msingi na sekondari zimejengwa, miradi mikubwa ya maji imejengwa na urasimishaji wa makazi na umilikishaji ukifanyika kikamilifu huku jimbo hilo likiongoza kwa zoezi hilo kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo

‘.. Yapo mambo mengi tumeyafanya kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ambayo hayakuwepo, Niwaombe ndugu zangu mtuchague tena mimi binafsi kuwa mbunge wenu, Mhe Rais Magufuli na madiwani ili tukatekeleze shughuli za maendeleo kutoka pale tulipoishi ..’ Alisema

Aidha Mgombea Ubunge huyo akaahidi kuendeleza michezo kwa wananchi hao kupitia mashindano aliyokuwa akiyaendesha ndani ya jimbo hilo yanayojulikana kama ‘The Angeline Ilemela Jimbo Cup’  huku akiwasisitiza kutouza viwanja kiholela na kutokacha zoezi la umilikishaji kwa faida yao binafsi na vizazi vyao.

Akimkaribisha mgombea ubunge huyo, Meneja Kampeni wa Jimbo la Ilemela Ndugu Kazungu Safari Idebe akawataka wananchi hao kuwapuuza wanasiasa wasiokuwa na nia njema wanaohubiri chuki, utengano na kukwamisha maendeleo kwani CCM kupitia mgombea wake wa Urais Dkt John Magufuli na Serikali yake wametekeleza shughuli kubwa ya kuwaletea waTanzania Maendeleo ikiwemo ukamilishaji wa miradi ya reli ya kisasa, mradi wa umeme wa Strigers Gorge, ununuzi wa ndege, ujenzi wa hospitali, zahanati na vituo vya afya.

Wakati Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Ilemela Ndugu Nelson Mesha akiwaomba wananchi hao kukiunga mkono chama chake na wagombea wake kwani wamebeba Ilani yenye dira na maono ya Tanzania wanayoitaka.

Kampeni za mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilemela kupitia CCM zitaendelea tena hapo kesho katika kata ya Kitangiri, viwanja vya Mihama jimboni humo.







No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages