LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 6, 2020

KINANA NA WAZIRI MKUU KATIKA MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM JIJINI ARUSHA

Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana akiwaomba wananchi wa Arusha wote Waichague CCM kwa kumpigia kura Mgombea Urais wa CCM Rais Dk. John Magufuli, Wabunge na Madiwani katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika siku ya Jumatano, Oktoba 28, mwaka huu, Wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM uliohutubiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa (kulia), katika Uwanja wa Relini jijini Arusha jana, Septemba 5, 2020.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 Mgombea Ubunge wa CCM katika Jimbo la Arusha, Mrisho Gambo wakati wa mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika katika Uwanja wa Relini jijini Arusha jana, Septemba 5, 2020
 Mgombea  ubunge wa CCM katika Jimbo la Arusha Mrisho Gambo (kulia)  akikumbatiana na Philemon Mollel (MONABAN) mmoja wa waliowania uteuzi wa CCM katika kugombea jimbo hilo.  Walikuwa katika Mkutano wa kampeni  uliohutubiwa na Mjumbe wa Kamti Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Tna Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa kwenye Uwanja wa Relini jijini Arusha, jana Septemba 5, 2020. Monaban alitamka hadharani kuwa hana kinyongo na Gambo na kwamba atashiriki kumpigia kampeni.
Wananchi wa jiji la Arusha wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa Relini, jana, Septemba 5, 2020. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages