Baadhi ya mambo muhimu yaliyosemwa katika mkutano wa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania DK. JOHN POMBE MAGUFULI Mjini SINGIDA leo Septemba 1, 2020.
#TZS bilioni 470.4 zimetumika kutekeleza miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Singida.
#Tumejenga vituo vya afya vilivyowezesha akinama 730 kufanyiwa upasuaji hivyo kuokoa maisha yao na watoto wao.
#Hospitali 3 za wilaya zimejengwa katika Wilaya za Mkalama, Ikungi na Singida.
#Katika kipindi cha miaka mitano viwanda zaidi ya 8,500 vimejengwa.
#Ajira milioni 6 zimezalishwa katika kipindi cha miaka mitano na katika kipindi cha miaka mitano ijayo tutazalisha ajira milioni 8
#TZS bilioni 52.6 zimetumika kujenga miundombinu ya shule yakiwemo madarasa, maabara na miundombinu mingine.
#Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida iko hatua za mwisho kukamilika ikiwa ni hatua mojawapo ya kuboresha sekta ya afya.
#Kulikuwa na Vijiji 2018 tu vilivyokuwa vimefikishiwa umeme mwaka 2015 lakini katika miaka mitano hii 2020 vijiji 9570 vimefikiwa kati ya vijiji 12280 nchi nzima.
#TZS bilioni 310 zimetumika kujenga miundombinu wezeshi.
#TZS bilioni 27.2 zimetumika kutekeleza miradi ya maji ipatayo 66.
#Uandikishaji wanafunzi umeongezeka kutoka milioni 1 hadi milioni 1.6 baada ya kuanza kwa mpango wa elimu bure.
#TZS bilioni 17 zimetumika kujenga barabara za Singida mjini na kuziwekea taa.
#Ujenzi wa barabara ya Chaya Singida hadi Tabora imebaki km 20 kukamilika.
#Vituo vya afya 487 vimejengwa Tanzania nzima.
#Tunajenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere litakalozalisha megawati 2,115.
#Vijiji 9,570 vimefikiwa na nishati ya umeme ikilinganishwa na Vijiji 2,018 vilivyokuwa na umeme mwaka 2015.
#Bajeti ya Wizara ya afya imeongezwa kutoka TZS bilioni 30 hadi TZS bilioni 270.
#Niko hapa kwa unyenyekevu mkubwa kuomba kura za vyama vyote kwa sababu maendeleo hayana chama.
#Visima 4 virefu vimechimbwa kuongeza upatikanaji wa maji.
#TZS bilioni 66 zimetumika kutekeleza miradi ya maji na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kutoka asilimia 41 hadi 54.
#Shule kongwe ikiwemo Mwenge Sec zimekarabatiwa ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha sekta ya elimu.
#Ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa TZS bilioni 850 hadi zaidi ya TZS Trilioni 1.5
#Tozo 114 zimefutwa katika sekta ya kilimo na wafanyabiashara ndogondogo wamefutiwa kodi 54.
# tumeweza kukusanya tsh trioni1.5-1.9 kwa mwezi ukilinganisha na Bilioni 850 zilizokuwa zikiikusanywa hapo awali.
#Kwa mujibu wa ripoti ya "Global Peace Index" Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki, ya 6 Afrika na 52 duniani kwa amani.
Mitandao ya simu imeimarika nchi nzima.
# Tumejenga ukuta wa km 25 eneo la Mererani ambao umesaidia kudhibiti wizi wa madini ya Tanzanite na upotevu wa mapato ya nchi.
#tunamshukuru Mungu kwa kutuepusha na janga la Corona kutokana na maombi tuliyofanya kama taifa. Hii imetoa somo kubwa kwa mataifa mengi duniani kuwa Mungu anaweza
*Imeandaliwa na John Mapepele, PIO- Singida
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇