LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 21, 2020

VULU: SERIKALI YA CCM ITASIMAMIA ZAIDI MAKUSANYO YA MAPATO YA NDANI AMBAYO ASILIMIA KUMI HUKOPESHWA VIJANA, WANAWAKE NA WENYE ULEMAVU

 Mgombea wa Ubunge Viti maalum mkoa wa Pwani Zainab Vulu


Na Scolastica Msewa, Kisarawe.

Mgombea wa Ubunge Viti maalum mkoa wa Pwani Zainab Vulu amewaomba wananchi kuwachagua wagombea wa CCM katika ngazi zote tangu ya Urais, Wabunge na Madiwani ili Serikali ya CCM iendelee kwa nguvu zaid kusimamia ukusanyaji mapato ya ndani ambayo asilimia 10 hutolewa kikopo kwa Vijana Wanawake na wenye na Ulemavu.


Hayo yamesemwa na Mgombea Ubunge viti maalum mkoa wa Pwani Zainabu Matitu Vulu wakati akiomba kura za kishindo kwa Wagombea wa CCM katika mkutano wa kampeni katika kata ya Msanga kijiji cha Bembeza na Msanga sokoni huko kisarawe mkoani Pwani.


Amesema CCM itakaposhinda na ataendelea kusimamia mapato ya halmashauri za mkoa wa Pwani ili kuimarisha kipato cha halmashuari ili ziwezekuendelea kutoa mikopo kwa akinamama, vijana na walemavu bila riba.


Amesema halmashauri nchini zimekuwazikitoa mikopo ambayo ni asilimia 10 ya mapato yake hivyo ili makundi hayo ya akinamama, vijana na walemavu wanufaike zaidi inabidi halmashauri nazo zisimamiwe kukusanya mapato yake ili fungu hilo la asilimia 10 la mapato liwe kubwa zaidi. 


Aidha Vulu amesema serikali inayoongozwa na CCM imefanya mengi katika sekta ya afya kwa kuimqarisha miundo mbinu, elimu na barabara hivyo ni sababu tosha kukipigia kura nyingi za kishindo ili kirejee madarakani kiendeleze mazuri iliyokwishaanza kuyafanya. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages