SERIKALI na wadau mbalimbali wameipogeza Benki ya NMB kwa msaada wake mkubwa wakulisaidia Taifa na wateja wake kukabiliana na changamoto za janga la COVID-19 ambalo athari zake kiuchumi na kibiashara zinaendelea kuitikisa dunia.
Pongezi hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha wakati wa hafla ya Mtandao wa Wateja Wakubwa wa Benki hiyo ‘NMB Executve Network’ uliyowaleta pamoja wateja zaidi ya 100 wa Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa mitatu ikiwemo Tanga na Kilimanjaro.
NMB ilitangaza unafuu wa ulipaji mikopo kwa wateja wake mwezi Mei mwaka huu, kupitia likizo ya marejesho ya mikopo yao na wengine wakiongezewa muda wa kulipa mikopo hiyo ili kuwasaidia kukabiliana na madhara yaliyoletwa na COVID–19 katika biashara zao.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Longido - Frank Mwaisumbe alisema NMB iliwasaidia sana wateja wake na imeendelea kuwa nao karibu wakati wote wa kipindi cha COVID-19 na wao kama Serikali wanawapongeza kwa hilo. Ni jambo kubwa hasa kwa Sekta ya Utalii ambayo imeathiriwa sana na COVID-19. Siyo hivyo tu, Frank vilevile aliipongeza Benki hiyo kwa utaratibu wake wa kukutana na wateja jambo ambalo alisema linasaidia kuboresha mahusinao kati ya Benki na wateja wao.
Washiriki wa kongamano la wafanyabiasha Wadogo na wa Kati waliojiunga na Mtandao wa NMB Business Club kutoka Arusha, Moshi na Tanga wakiwa katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.
Tangu kuanzishwa kwa NMB Business Club miaka sita iliyopita, mtandao huo upo kwenye Mikoa ya; Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Mtwara, Mbeya na Dodoma huku washirika wake wakiwa zaidi ya 600.
Mwakilishi wa kiwanda cha ngozi cha Tanneries kutoka Himo Wilaya ya Moshi - France Sawerio kulia,akitoa maelezeo kwenye maonesho ya bidhaa anazo zitengeneza,wakati Viongozi wa Benki ya NMB walipo tembelea banda lake wakati wa Kongamano la wafanyabiashara Wadogo na wa Kati (NMB Business Club), lililofanyika katika ukumbi wa Kuringe - mjini Moshi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇