Na Lydia Lugakila, Kagera
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba Mkoani Kagera imewahukumu watu wawili kunyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani kwa kuhusika na mauaji ya mtu mmoja katika eneo la Kitendaguro katika Manispaa ya Bukoba yaliyotokea Machi 9, 2015, huku mmoja akiachiwa huru.
Hukumu hiyo ya kesi namba 34 ya mwaka 2020 imetolewa na Jaji wa Mahakama hiyo Sam Rumanyika baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo dhidi ya watuhumiwa hao.
Akizungumza baada ya hukumu hiyo Mkurugenzi wa usimamizi wa kesi na uratibu wa upelelezi, kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Hashimu Ngole amesema Serikali imeridhishwa na maamuzi ya Mahakama ambayo yanarejesha imani ya wananchi waliokuwa wakiishi kwa wasiwasi kwa kuhofia kukatwa makoromeo.
Mwaka 2015 yaliibuka mauaji ya kukata watu makoromeo na kuzua hofu kwa wakazi kwa baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Kagera.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇