LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 9, 2020

WASHINDI WATUNUKIWA TUZO MAONESHO YA NANENANE YA KANDA YA KATI DODOMA


Wananchi wakiwa wamesongamana kugombea kuingia kwenye viwanja vya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati vilivyopo Nzuguni, jijini Dodoma. Kiingilio kilikuwa sh. 1000 kwa wakubwa na watoto sh. 500. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-CCM BLOG


Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi akiwakabidhi  wawakilishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kombe la Ushindi wa Pili wa Jumla wa Maonesho ya Nanenane ya Kanda ya Kati jijini Dodoma.

 


Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stelah Ikupa akikabidhi cheti na Kombe kwa wawakilishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambayo imepata ushindi wa kwanza wa Paredi ya Wanyama



Meneja Masoko wa Kampuni ya Mkaa Mweupe, Aristotre Nikitas akipokea cheti ushindi wa pili wa kundi la Wajasiriamali na Wawekezaji Wadogo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stelah Ikupa 


Julius Soniga akikabidhiwa cheti cha ushindi wa tatu katika kundi la Ufugaji Bora katika maonesho hayo

Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stelah Ikupa akimpongeza Kiongozi Msanii wa Kikundi cha Ngoma cha Mwinamila kiichotumbuiza maonesho hayo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stelah Ikupa  akihutubia katika hafla za kunga rasmi maonesho hayo

Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga (kushoto)  na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo,Zahara Michuzi  wakifurahia Mkulima kutoka wilaya hiyo, kupata cheti cha ushindi  wa Mkulima Bora katika Maonesho hayo.

Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Steah Ikupa akiwakabidhi maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii, cheti cha ushindi wa kwanza kundi la Wizara Sekta ya Uchumi Uzalishaji katika maonesho hayo yaliyofikia kilele leo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa wizara hiyo. Doreen Makaya.

Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Steah Ikupa akikabidhi cheti cha ushindi wa tatu  wa Bodi za Mazao na Mifugo kwa mwakilishi wa Bodi ya Mtama.


 Wakuu wa Wilaya za mikoa ya Dodoma na Singida wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhudhuria kufungwa rasmi kwa  Maonesho ya Wakulima ya Nanenane ya Kanda ya Kati, yaliyofungwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulmavu), Stelah Ikupa kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodma 

Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stella Ikupa akimkabidhi cheti Meneja wa Kanda ya Kati Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Stella Rutaguza katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kanda ya Kati Dodoma. Kulia kwake ni Afisa Bima Mwandamizi wa TIRA. Adam Maneno. Tira imepaata ushindi wa pili wa Mamlaka za Huduma na Udhibiti.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages