ALIYOAHIDI AMETEKELEZA
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mikono wananchi ikiwa ni ishara ya kuwasalimia alipowasili kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, ambapo aliahidi kuboresha kiwanda cha kukoboa kahawa na kujenga barabara ya lami kutoka Mbinga hadi Mbamba bay.
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye uwanja wa Majimaji ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa Serikali yake itafanyakazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi akiwaomba wananchi wa Ruvuma kumpigia kura Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM kwenye Uwanja wa Maji Maji Mjini Songea, mkoani Ruvuma. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM,, dK John Magufuli akiwa na watoto aliowapatia zawadi alipokuwa akiondoka baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma
Mwananchi akimpigia makofi Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli baada ya kufurahishwa na hotuba yake katika Kijiji cha Kigonsera, wilayani Mbinga, Ruvuma.
Dk Magufuli akisalimiana na dada wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyasa kupitia CCM, na mhamasishaji Mkuu wa CCM, marehemu Kapteni John Komba, alipokwenda kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni Komba katika Kijiji cha Lituhi, wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma akiwa katika ziara ya kampeni za urais, ubunge na udiwani
Dk Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Kapteni Komba
Dk Magufuli na viongozi wengine wa CCM, wakiomba dua kwenye kaburi la marehemu Kapteni Komba
Ngoma ikitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni za urais, ubunge na udiwani katika Kijiji cha Lituhi, Wilaya ya Nyasa
Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Mji wa Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Ruvuma
Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi
Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli
Dk Magufuli akimvisha kofia ya CCM, aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kijiji cha Kwanza Kata ya Lituhi, kupitia Chadema, Sixbert Nyembo baada ya kutangaza kuwa yeye na wenzie zaidi ya 270 kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Lituhi, wilayani Nyasa.
Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli wakati msafara wake ulipozuiwa katika Kijiji cha Rwanda, wilayani Mbinga
Wananchi wakishangilia katika Kijiji cha Amani walipomuona Dk Magufuli wakati msafara wake ulipozuiwa katika Kijiji hicho kilichopo wilayani Mbinga
Msafara wa Dk Magufuli ukipita kwenye Barabara mpya ya lami inayotoka Songea kwenda Mbinga
Dk Magufuli akishangiliwa alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Kigonsera waliomzuia alipokuwa akienda kwenye kampeni mjini Mbinga
Dk Magufuli akiwasamia wananchi alipowasili kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga
Dk Magufuli akihutubia wananchi na kutoa ahadi mbalimbali atakazozitekeleza akichaguliwa kuwa rais.
Dk Magufuli akimkabidhi Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda Ilani ya Uchaguzi ya CCM wakati wa mkutano huo wa kampeni
Dk Magufuli akionesha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kabla ya kumkabidhi mgombea ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini wakati wa mkutano huo
Dk Magufuli akimsalimia mmoja wa walemavu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga
Sehemu ya wananchi walioshiriki kwenye mkutano wa kampeni za CCM katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma leo
Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni katika Jimbo la Peramiho
Mama mfuasi wa CCM akifurahi baada ya kumsikia Dk Magufuli akiahidi kuanzisha pensheni kwa wazee kuanzia mwakani
Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni.
Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM, Dk. John Magufuli akiwapungia mkono wananchi kuwaaga baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma
Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwapungia mkono wananchi kuwaaga baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma
Sehemu ya wanchi wa Ruvuma wakinyoosha mikono kukubali kumpigia kura Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa MajiMaji mjini Songea
Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu nchini, Amon Mpanju akiwashutumu viongozi wa upinzani akiwemo mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba Wananchi Ukawa, Edward Lowassa kwa kitendo chake cha kuwadhihaki walemavu. Mpanju alikuwa akihutubia katika mkutano wa kumnadi Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye uwanja wa majimaji ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa Serikali yake itafanyakazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇