LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 31, 2020

SIMBACHAWENE AJINADI, AMUOMBA RAIS MAGUFULI WAJENGEWE BARABARA YA LAMI JIMBO LA KIBAKWE

Mgombea ubunge Jimbo la Kibakwe kupitia CCM, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akipokea kitabu cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali baada ya kujinadi yeye na Mgombea Urais wa Tanzania wa chama hicho, Dk. John Magufuli, wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM, kwenye Uwanja wa Jamhuri, DODOMA Agosti 29, 2020. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

Simbachawene akijinadi kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM ambapo alimuomba Rais Magufuli ambaye ndiye mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, kujengewa barabara ya lami katika jimbo hilo.

Viongozi wanaomsikiliza kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli, Makamu Mwenyekiti na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Simbachawene akifurahi kukabidhiwa  na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali, Ilani ya CCM ya Uchaguzi.


Simbachawene akiondoka jukwaani baada ya kukabidhiwa kitabu cha Ilani.



 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages