LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 10, 2020

POLISI YADHIBITI HALI YA MAMBO BELARUS

Polisi nchini Belarus wamefanikiwa kudhibiti hali ya mambo, wakati waandamanaji wa upinzani walipoingia mitaani, baada ya uchaguzi tete wa urais ambao wakosoaji wanasema ulivurugwa.


Shirika la habari la serikali la Belta lilimnukuu waziri wa mambo ya ndani mapema hii leo, kufuatia makabiliano kati ya polisi na waandamanaji katika mji wa Minsk.

Washuhudiaji waliliambia shirika la habari la AFP kwamba watu kadhaa walijeruhiwa na baadhi ya picha za kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha nyuso zao zimejaa damu.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani alipoulizwa na AFP kuhusu taarifa hizo, alikataa kusema iwapo kuna mtu aliyejeruhiwa .

Matokeo ya awali yanampa ushindi kiongozi wa muda mrefu, Alexander Lukashenko kwa asilimia 79.7 ya kura zote na kurejea mamlakani kwa awamu ya sita, huku mpinzani wake Svetlana Tikhanovskaya, akishika nafasi ya pili kwa asilimia 6.8.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa usiku.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages