|
Mgombea ubunge Jimbo la Chamwino, Deo Ndejembi (kushoto), akipokea kitabu cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali baada ya kujinadi yeye na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli, wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM, kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Agosti 29, 2020. Jimbo hilo ndipo ilipo Ikulu ya Rais. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA |
|
Ndejembi, ambaye pia alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, akijinadi kwa wananchi ili achaguliwe katika jimbo hilo, apate fursa ya kuliongoza kwa umakini na kuliletea maendeleo makubwa. Pia amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumpigia kura nyingi za ndiyo Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais John Magufuli katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28,2020. Anayemsikiliza kulia ni Rais John Magufuli. |
Ndejembi ameahidi kushirikiana na uongozi wa chama pamoja na wananchi wa jimbo hilo kufanya kampeni za nguvu ili washinde urais, ubunge na udiwani ili kuipa heshima Ikulu.
Wanaomikiliza Ndejembi kutoka kulia ni; Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Phillip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali, Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Raiss wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇