Na
mwandishi wetu, Geita
Shirika
la umeme Tanzania (TANESCO) kupitia idara ya masoko, limeendelea na kampeni yake ya kutoa elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wamiliki
wa migodi na wamiliki wa mashine za
kusaga na kukoboa nafaka safari hii mkoani Geita.
Migodi
iliyotembelewa na kikosi kazi hicho cha TANESCO ni pamoja na Migodi ya Geita
mjini, Wilaya za Nyanghwale na Bukombe, lakini
pia mashine za posho mills
zilizotembelewa ni za Buseresere Kasamwa, Nyanghwale,Bukombe, Katoro na Geita
mjini.
Kwa
mujibu wa Eng Ally Koya kutoka kitengo cha masoko Tanesco makao makuu alisema lengo
hasa la kampeni hiyo ni kuwawezesha kufahamu
jinsi ya kupunguza gharama ambazo si za lazima kwa kununua vifaa vya
kisasa na kuachana na vifaa
vilivyochakaa na vya zamani kwani vinatumia umeme mwingi.
Wamiliki
hao walielimishwa kuhusu utaraibu wa kufunga motor za kisasa na kuzifanyia service
mara kwa Mara ili motor iendelee kuwa
na ufanisi.
“Matumizi
bora na sahihi ya umeme ni muhimu kwa usalama kwani umeme ni nzuri kama ukiutumia kwa kuzingatia usalama
lakini pia umeme ni moto mara moja.” Alisema Mhandisi Koya
Walipewa
pia elimu ya kufunga power factor ili
iweze kuwasaidia uendeshaji wa mitambo yaani kVA haitakuwa kubwa.
Aidha
wamiliki wa migodi na mashine walishukuru ujio wa wataalamu hao wa TANESCO
kwani umewaongezea uelewa na hivyo kuongeza ufanisi katika eneo la matumizi
sahihi ya nishati hiyo ya umeme.
No comments:
Post a Comment
ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇