Na Mwandishi Wetu, Nanyumbu
KAMPENI ya kuhamasisha wanachi kutumia nishati ya umeme inayoratibiwa na idara ya masoko ya SHIRIKA la umeme Tanzania TANESCO makao makuu imetua mkoani Mtwara.
Maafisa wa TANESCO wakiongozana na Meneja wa TANESCO wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Mhandisi Sidala Maeda wametembela vijiji kadhaa vikiwemo vya Liputi, Raha leo na Namyomyo na baadaye timu iliungana na Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Nanyumbu Mhandisi Peter Mwaimu na kufika vijiji vya Tuungane, Mtalikachao
Timu hiyo ikiwa kwenye vijiji hivyo ilifanya mikutano na wananchi na kutoa elimu kuhusu matumizi bora na sahihi ya umeme, faida itokanayo na nishati ya umeme ikiwa ni pamoja na kuwahamishwa wanachi kutumia nishati hiyo kujiletea maendeleo.
“Lakini pia tumetoa elimu ya jinsi ya kuwaunganishia umeme wana vijiji katika wilaya hizo kwa gharama nafuu ya Shilingi elfu ishirini na saba tu ( 27,000/=).” Alisema Mhandisi Maeda.
Alisema wananchi wote wataunganishiwa umeme kwa wakati hivyo basi aliwasisitiza kufanya mtandao (wire ring) ndani ya nyumba zao kwa kuwatumia wakandarasi waliosajiliwa na kuepuka vishoka.
Wilaya ya masasi pekee ina jumla ya vijiji 67 kati ya vijiji hivyo 43 tayari vineshanufaika kwa kuwashiwa umeme.
Afisa Masoko TANESCO makao makuu Bi. Jennifer Mgendi (kulia) akielezea wananchi wa Tuungane kifaa cha UMETA au umeme tayari ambacho hutumika badala ya wiring, wale ambao hawatafanya wiring watumie kifaa hicho |
Afisa masoko TANESCO makao makuu Bi. Jennifer Mgendi akielezea taratibu za kuunganishiwa umeme kwa kwa gharama nafuu ya Shilingi 27,000/= tuu na kuwashauri wananchi kutumia wakandarasi waliosajiliwa katika Kijiji Cha Raha leo wilaya ya Masasi mkoani Mtwara
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇