LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 12, 2020

KAMPENI YA KUUNGANISHA UMEME VIJIJINI KWA BEI NAFUU YA SH. 27,000 YAHAMIA NANYUMBU NA MASASI

Na Mwandishi Wetu, Nanyumbu

KAMPENI ya kuhamasisha wanachi kutumia nishati ya umeme inayoratibiwa na idara ya masoko ya SHIRIKA la umeme Tanzania TANESCO makao makuu imetua mkoani Mtwara.


Maafisa wa TANESCO wakiongozana na Meneja wa TANESCO wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Mhandisi Sidala Maeda wametembela vijiji kadhaa vikiwemo vya Liputi, Raha leo na Namyomyo na baadaye timu iliungana na Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Nanyumbu Mhandisi Peter Mwaimu na kufika vijiji vya Tuungane, Mtalikachao


Timu hiyo ikiwa kwenye vijiji hivyo ilifanya mikutano na wananchi na kutoa elimu kuhusu matumizi bora na sahihi ya umeme, faida itokanayo na nishati ya umeme ikiwa ni pamoja na kuwahamishwa wanachi kutumia nishati hiyo kujiletea maendeleo.


“Lakini pia tumetoa elimu ya jinsi ya kuwaunganishia umeme wana vijiji katika wilaya hizo kwa gharama nafuu ya Shilingi elfu ishirini na saba tu ( 27,000/=).” Alisema Mhandisi Maeda.


Alisema  wananchi wote wataunganishiwa  umeme kwa wakati hivyo basi aliwasisitiza kufanya  mtandao (wire ring)  ndani ya nyumba zao kwa kuwatumia wakandarasi waliosajiliwa na kuepuka vishoka.


Wilaya ya masasi pekee ina jumla ya vijiji 67 kati ya vijiji hivyo 43 tayari vineshanufaika kwa kuwashiwa umeme.


Kwa upande wake Meneja wa TANESCO wilaya ya Nanyumbu Bw. Peter Mwaimu licha ya kuwahamasisha wananchi kutumia nishati ya umeme lakini pia amewaelimisha kuhusu matumizi salama ya umeme ili kuepuka athari za matumizi umeme yasiyozingatia usalama.
++++++++++++++++++++++


Afisa Masoko TANESCO makao makuu Bi. Jennifer Mgendi (kulia) akielezea wananchi wa Tuungane kifaa cha UMETA au umeme tayari ambacho hutumika badala ya wiring, wale ambao hawatafanya wiring watumie kifaa hicho
Wananchi wa Mtalikachao wakimsikiliza meneja wa TANESCO wilaya ya Nanyumbu (hayupo pichani) Bw. Peter Mwaimu akiwaeleza jinsi miradi ya umeme vijijini inavyoendelea na kuwaelezea usalama wa umeme na athari zake

Afisa masoko TANESCO makao makuu Bi. Jennifer Mgendi akielezea taratibu za kuunganishiwa umeme kwa kwa  gharama nafuu ya Shilingi 27,000/= tuu na kuwashauri wananchi kutumia wakandarasi waliosajiliwa katika Kijiji Cha Raha leo wilaya ya Masasi mkoani Mtwara

 Meneja wa TANESCO wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Mhandisi Sidala Maeda akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namyomyo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages