Mgombea ubunge Viti Maalumu Umoja wa Vijana CCM, Mariam Ditopile akipokea kitabu cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali baada ya kujinadi yeye pamoja na Mgombea Urais wa Tanzania wa CCM Dk. John Magufuli, wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM, kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Agosti 29, 2020. Wanaomfurahia kushoto ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete. Kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Ditopile ameahidi kuhamasisha vijana, wanachama, viongozi na wananchi kufanya kampeni za nguvu kuhakikisha madiwani, wabunge na Rais wa CCM wanashinda kwa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.
Viongozi wakimsikiliza kwa makini Ditopile alipokuwa akieleza mikakati ya kampeni kuhakikisha ushindi mkubwa kwa CCM unapatikana. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu, Dk. Bashiru Ali, Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli, Makamu Mwenyekiti na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete.
Ditopile akiondoka baada ya kukabidhiwa Kitabu cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇