Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, Mathayo Masele akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi la Benki ya NMB Malinyi. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Mikopo waa NMB, Demetus Kaguna, Mwakilishi wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Salie Mlay, Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Dismas Prosper na Meneja wa Tawi la Malinyi, Ipyana Mwakatobe.
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mathayo Masele na Kaimu Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB Salie Mlay wakipiga makofi baada ya kufunguliwa rasmi kwa tawi la Benki ya NMB Malinyi.
Benki ya NMB imeendelea kupanua wigo wake kwa kufungua tawi ‘NMB Malinyi’ katika wilaya ya Malinyi
Mkoani Morogoro. Ufunguzi wa tawi hili umeleta ahuweni kwa wakazi waliokuwa
wanasafiri umbali wa kilomita 160 kwenda mji wa Ifakara Wilayani Kilombero
kupata huduma za kibenki.
Masele alisema kuwa Benki hiyo licha ya kukuza uchumi pia itawapunguzia
gharama wafanyabishara, na Taasisi ambazo zilikuwa zikitumia gharama kubwa
kwaajili ya kusafirisha fedha kwa usalama zaidi
Mwakilishi wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB - Salie Mlay, alisema
moja ya kichocheo kikubwa cha kufungua tawi hilo ni kuwasaidia wakulima na
wafugaji waweze kupata mikopo pamoja na elimu ya ushirika utakaowapa tija kwa
kutumia mfuko wa NMB Foundation.
Sambamba na uzinduzi huo, NMB
imetoa msaada wa vifaa vya ujenzi vikiwemoa mabati, kofia, misumari na mbao kwaajili
yakukamilisha uwezekaji vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Nawigo
iliyopo Malinyi. Ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇