Akihutubia taifa juu ya mkakati wa taifa wa kudhibiti maambukizi ya Covid-19 Rais Uhuru amesema amri ya kutotembea kati ya saa tatu usiku na saa kumi alfajiri itaendelea kwa siku 30.
" Hakutakua na mauzo ya pombe katika baa au katika migahawa " kwa kipindi hicho.
Rais Kenyatta. amewataka wamiliki wa vilabu vya pombe kuunda mbinu za udhibiti wa shughuli yao kama sehemu ya wajibu wao kama raia kwa wateja wao ili kusaidia mchakato wa kufunguliwa kwa biashara yao.
Hotuba hii imetolewa kufutia kikao cha kamati ya taifa ya dharura.
Amesema masharti ya uuzaji wa mitumba yametolewa na mwongozo utatolewa juu ya biashara hiyo na serikali yake
Bwana Kenyatta pia amesema pia amewapongeza Wakenya kwa kufuata masharti ya kukabiliana na Covid-19, akisema kuwa kwasasa kiwango cha maambukizi nchini humo kimeshuka kutoka asilimia 13 mwezi Juni hadi asilimia 8 mwezi wa Agosti.
Hotuba ya rais inatolewa huku maambukizi mapya ya virusi yakiripotiwa kufikia 213 katika kipindi cha saa 24 na kulifanya taifa hilo kuwa na jumla ya visa 33,016. Vifo 5 pia vimeripotiwa leo na hivyo jumla ya watu waliokufa kufikia 564. Waliopona virusi vya corona ni zaidi ya 19,000.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇