LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 10, 2020

WANANCHI WAFURIKA BANDA LA KIKUNDI CHA KILIMO BIASHARA MAPATO VIWANJA VYA SABASABA

 Mjasiliamali kutoka Geita Wilaya ya Bukombe na Mkurugenzi wa Kilimo Biashara  Mapato, Veronica Manala (kushoto) akiwaelezea wateja wake jinsi Chia Seed inavyo okoa maisha ya watu mara walipotembelea Banda la Chama Cha Wafanya Biashara Wanawake Tanzania (TWCC) katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa Julai 10, 2020 Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).

NA KHAMISI MUSSA:. 


Chia Seed ni zao geni ambalo tumelitoa Nchi ya Uganda ambapo asili ya zao hili limetoka 

Nchini Mexico na nizao linalotokana na mme unaojulikana kitaalam Salvia Hispanica, likikuwa linavirutubisho vyote, linamadini ya aina zote hivyo Chia Seed ni Afya yako Maisha yako.

Hayo yamesemwa na  Mjasiliamali kutoka Geita na Mkurugenzi wa Kilimo Biashara  Mapato, Veronica Manala wakati wananchi walivyo miminika kutaka kujuwa zao hilo linavyo weza okoa maisha ya watu mara walipotembelea Banda la Chama Cha Wafanya Biashara Wanawake Tanzania (TWCC),  Maonesho ya 44 ya Kimataifa viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa Dar es Salaam.


Manala alisema, wao hasa wamejikita katika utengenezaji na wauzaji wa vyakula vya asili ikiwemo Chia Seed na unga wake, ubuyu na unga wake, karanga zilizo kaangwa, mbogamboga zilizo kaushwa, kisamvu na matembele ambapo alisema.


Chia Seed inakusaidi kutoa mafuta yasiyo yalazima mwilini, hivi vitambi kutokana na vyakula tunavyo kula hasa chipsi si chakula cha kiafrika, kutumia mbegu za maboga na akawashuri wananchi hao kuwa turudi nyumbani kumenoga. 


Kama anavyo sisiza Baba yetu Magufuli na anatushauri hivyo kula vyakula vyetu vya asili, jamani tufanye hivyo pia nitoe wito kwa Watanzania tutumie vyakula vya asili ikiwemo mbegu za maboga, mbegu za ubuyu na Chia Seed inamanufaa chungu mzima, iwe kwa watoto, iwe kwa wazee na kwa rika zote karibuni tuzidi imarika kwa afya zetu

Wananchi wakimsikiliza Mjasiliamali kutoka Geita Wilaya ya Bukombe na Mkurugenzi wa Kilimo Biashara  Mapato, Veronica Manala. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages