Wiki liyopita, bunge la Chad liliidhinisha mswada wa kumfanya Idrissa Deby Itno kutoka kuwa jenerali hadi Jemadari Mkuu - cheo cha juu kabisa ya jeshi nchini humo.
Cheo hicho kinachukuliwa kama kichocheo cha kutaka madaraka na ya kudumu.
Idrissa Deby hakuwa rais wa kwanza kuingia madarakani hata kabla ya kuingia rasmi kama rais.
Lakini unajua kwamba Idrissa Deby sio kiongozi wa kwanza barani Afrika kutaka kuwa na cheo kitakachomwezesha kuendelea kuwa na madaraka hadi kifo chake?
BBC inaagazia baadhi ya viongozi wa Afrika ambao wamefikia hatua ya Jemadari Mkuu ama kwa kujipandisha ngazi wenyewe au kwa kupitia sheria za bungeni.
Idi Amin Dada - Uganda
Idi Amin Dada, aliyekuwa rais wa Uganda, alizaliwa 1925 huko Koboko kaskazini mashariki.
Alisomea nchini humo na kuwa mwanajeshi katika jeshi la Uingereza 1945.
1966 alichaguliwa kama kamanda wa jeshi la Uingereza chini ya ukoloni.
Alikuwa rais 1971 baada ya kupinduliwa kwa rais wa kwanza aliyechaguliwa Milton Obote na kuongozi nchi hiyo kwa miaka minane.
1979, alilazimika kutoroka Uganda kutokana na ghasia zilizotokea nchini humo na kukimbilia Saudi Arabia, ambapo aliaga dunia huko, 2003.
Lakini alikuwa amejipatia nafasi ya kuwa jemedari mkuu 1975, cheo cha juu zaidi katika jeshi la Uganda cha nyota tano.
Kule Magharibi, anachukuliwa kama Dikteta aliyeyumbisha uchumi wa Uganda.
Mohamed Hussein Tantawi - Misri
Mohamed Tantawi aliazaliwa eneo la Wanubi kati ya Misri na Sudan 1935, na baada ya kuhitimu masomo aliingia jeshini 1956.
Alikuwa rais wa Misri baada ya kuanguka kwa utawala wa rais Mubarak Februari 11, 2011 na kujiuzulu Juni 30, 2012.
Alipokea shahada ya kwanza akiwa chuo cha kijeshi, ambapo alisomea sayansi ya maswala ya kijeshi na kujifunza mambo mengi ya kijeshi.
Kwa zaidi miaka 50 ameshiriki katika vita ya Misri ikiwemo mashambulizi ya 1967 na 1973 Mashariki ya Kati, hapo akapata cheo cha Jemedari Mkuu.
Mwaka 1191, kufuatia Iraq kuvamia Kuwait, ilikuwa sehemu ya vikosi vya muungano katika vita ya kwanza ya Ghuba. Amepokea tuzo za heshima kutoka Misri, Kuwait na Saudi Arabia.
Aliteuliwa kama waziri wa ulinzi mwaka huo huo.
Mohamed Hussein Tantawi anachukuliwa kama mfuasi wa aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak.
Jean-BĂ©del Bokassa - Jamhuri ya Afrika ya Kati
Bokassa alizaliwa Februari 22, 1921, huko Bobangui, M'Baka, kijiji cha Lobaye.
Alisoma Brazzaville, na akataka kuwa mhubiri lakini baadae akashawishiwa na wazazi wake kujiunga na jeshi la Ufaransa wakati wa ukoloni.
Baada ya kuhitimu 1939, alisajiliwa jeshini na kuwa mwanajeshi 1941 na kushiriki vita dhidi ya vikosi vya Wanazi.
Januari, 1962 Bokassa aliondoka jeshi la Ufaransa na kuijiunga na jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati kama kamanda.
Alihudumu kama rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ya mwaka 1966 na mwaka 1976 alikuwa kiongozi wa jeshi.
Baadae akajitangaza kama mtawala wa Jamhuri ya Afrika ya Kati 1976 na kubadilisha jina la nchi hiyo hadi Milki ya Afrika ya Kati.
Alikosolewa na jumuiya ya kimataifa kwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya watoto 100 wa shule na kusababisha kifo chake kilichotekelezwa na wanajeshi wa Ufaransa.
Alitorokea CĂ´te d'Ivoire na kurejea Ufaransa.
Baadae alirejea Jamhuri ya Afrika ya Kati, 1980, akafunguliwa mashtaka na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
2003 aliachiliwa kwa msamaha wa rais kusherehekea miaka hamsini ya uhuru.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇