LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 7, 2020

TUJIKUMBUSHE KAMPENI ZA MAGUFULI 2015; NITABORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA-MAGUFULI (Aliyoyahidi ametekeleza)

NITABORESHA MASLAHI YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA-MAGUFULI

SEPTEMBA 8, 2015: Msafara wa Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili katika mkutano wa hadhara wa kampeni, Korogwe vijijini.
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk.John Magufuli akifafanua jambo kwa

msisitizo huku akibainisha kuwa iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu

mwaka huu, basi Serikali yake itahakikisha inaboresha maslahi ya watumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini kutokana na kutambua
mchango wao katika kulinda amani ya nchi yetu.

Dk. Magufuli alisema kuwa anataka kuona watumishi wa jeshi hilo wanakuwa na mishahara
mizuri na hiyo itawezesha kufanya kazi ya ulinzi na usalama wa nchi kwa
ufanisi zaidi huku akitumia nafasi hiyo kuomba Watanzania kudumisha
amani ya nchi kwani ikipotea hakutakuwa na maendeleo ya aina yoyote.

Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo leo  katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Korogwe,
Mkinga na Lushoto ikiwa ni sehemu ya mikutano ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa rais ambapo alisema anatambua kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama na kuongeza kuwa serikali yake itaboresha
maslahi ya wanajeshi wa majeshi yote Nchini . 
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli

wakiwaaga wananchi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa

kampeni uliofanyika mjini humo jioni ya leo.
Mgombea wa Urais kupitia CCM,  Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa

Lushoto kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jitegemee.
  Lushoto ikiwa imefurika watu tayari kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa

hadhara  katika uwanja wa Togotwe-Mponde Bumbuli kuwahutubia

wananchi na kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge

jimbo la Bumbuli, January Makamba kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba akisisitiza jambo kwa

Wananchi wake katika jimbo la Bumbuli jioni ya leo kwenye mkutano wa

kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
 Wakazi wa Jimbo la Bumbuli wakifuatilia kwa makini mkutano wa Mgombea wa Urais

kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa

kata ya Magoma wakati akiwa njiani kuelekea Korogwe mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa

Mashewa wilayani Korogwe kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo

aliwaambia wananchi hao kuwa serikali yake itakuwa ya kuchapa kazi kwa
maendeleo ya wananchi na nchi kwa jumla.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa

Jimbo la Korogwe Vijijini Ndugu Stephen Ngonyani kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kwamazandu, Korogwe Vijijini.
Bangozzzz
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge

wa Jimbo la Korogwe mjini,  Mary Chatanda Ilani ya uchaguzi ya CCM

kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Chuo cha Ualimu Korogwe.
Mwenyekiti wa Wazazi CCM Taifa, Ndugu Bulembo akimkaribisha mgombea Urais wa CCM

Dk. John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi katika uwanja wa Togotwe-Mponde wilayani humo.
Wakazi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni wa CCM jioni ya leo,
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa

Bumbuli kwenye viwanja vya Togotwe ambapo aliwaahidi kuwajengea barabara ya lami pamoja na kufuatilia suala la kiwanda cha Chai cha Mponde.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa

Bumbuli kwenye viwanja vya Togotwe ambapo aliwaahidi kuwajengea barabara

ya lami pamoja na kufuatilia suala la kiwanda cha Chai cha Mponde.
Wananchi wakifuatilia mkutano.
  Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akifafanua jambo mbele ya umati wa wananchi  wa

Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya

Togotwe.
Wananchi wa Lushoto mjini wakishangilia jambo mara baada ya kumsikia Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia .




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages