LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 3, 2020

TETESI ZA SOKA ULAYA JULAI ,2020

Mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann

Maelezo ya picha,
Mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann
Changamoto zinazomkabili mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann zinaweza kufanya Arsenal au Inter Milan kupata nafasi ya kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 29. (Express)
Arsenal wana matumaini kuwa beki wa kati David Luiz 33, anaweza kujaribu kumshawishi Mbrazili mwenzake Thiago Silva,35, kujiunga na klabu baada ya kuondoka Paris St-Germain msimu huu. (Le 10 Sport, via Mail)
Washika bunduki wameongeza juhudi za kumuwinda kiungo wa Atletico Madrid, Thomas Partey lakini hawako tayari kufikia dau
Maelezo ya picha,
Washika bunduki wameongeza juhudi za kumuwinda kiungo wa Atletico Madrid, Thomas Partey lakini hawako tayari kufikia dau
Washika bunduki wameongeza juhudi za kumuwinda kiungo wa Atletico Madrid, Thomas Partey lakini hawako tayari kufikia dau linalotakiwa la pauni milioni 45. (Athletic, via Mirror)
Mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga katika klabu ya Chelsea Andreas Christensen, 24, amesema hana nia ya kuondoka kwenye klabu na yuko tayari kwa mkataba mpya ndani ya Stamford Bridge. (Goal.com)
Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan huenda akajiunga na Roma
Maelezo ya picha,
Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan huenda akajiunga na Roma
Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan, 31, anaonekana kujiandaa kujiunga na Roma kwa mkataba wa kudumu baada ya mkataba wa kucheza kwa mkopo katika klabu ya ligi ya Serie A kuongezwa. (Mail)
Winga wa Liverpool Mohamed Salah, 28, amesema anataka kusalia kwenye klabu hiyo ''kwa muda mrefu''. (Bein Sports, via Express)
Winga wa Liverpool Mohamed Salah, 28, anataka kusalia kwenye klabu hiyo
Maelezo ya picha,
Winga wa Liverpool Mohamed Salah, 28, anataka kusalia kwenye klabu hiyo
Kinda wa Manchester United Mbelgiji Largie Ramazani, 19, amekataa kusalia Old Trafford akiwa tayari kuhamia Almeria ya Uhispania. (Manchaster Evening News)
Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Rennes Florian Maurice amesema kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumuuza kiungo Eduardo Camavinga, 17 anayecheza timu ya vijana wa chini ya miaka 21. (AS)

1 comment:

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages