Angelina Mabula sasa haliwezi kuwa jina geni tena miongoni mwa mamilioni ya Watanzania na kwingineko Duniani.
Ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambaye kwa aliyefuatilia kwa karibu utendaji kazi wake, atakubali kwamba ni mwanamke mchapakazi ambaye amefanikiwa kulifanya jimbo hilo kunawiri kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na zamani.
Pamoja na jimbo hili kujipatia Mbunge Mwanamke ambaye ni mchapakazi, lakini limebahatika pia kuwa miongoni mwa majimbo ambayo yana kiongozi mwenye hadhi ya Naibu Waziri, maana Angelina Mabula pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye hakika ameweza kuendana na kasi ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.
Angelina amefanya mengi sana ya kupigiwa mfano katika Kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, na kama ilivyo ada, Wabunge wote ambao ni wa CCM hutayarisha Taarifa zao za Utekelezaaji wao wa Ilani ya CCM jimboni na kuiwasilisha Makao Makuu ya CCM.
Kwa kuwa Blog hii ya Taifa ya CCM imebahatika kuipata taarifa hiyo ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Angelina Mabula ya kipindi cha Oktoba 2015 hadi Juni 2020, tumeichapisha ili na wewe mdau uweze kuisoma taarifa hiyo, hatua kwa hatua. Kuisoma...BOFYA HAPA
Your Ad Spot
Jul 2, 2020
Home
featured
siasa
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM 2015-2020 YA MBUNGE ANGELINA MABULA, JIMBO LA ILEMELA MKOANI MWANZA
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM 2015-2020 YA MBUNGE ANGELINA MABULA, JIMBO LA ILEMELA MKOANI MWANZA
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Hakika mama amejitahidi sana,said endelea moyo wa kiuzalendo uliolelewa na CCM,ili kuendelea kufanya vizuri zaidi
ReplyDelete