MSHAMBULIAJI wa kimatafa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza kwa dakika 80 timu yake, Aston Villa ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Villa Park.
Kwa ushindi huo, Aston Villa inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 35 na kujiinua kwa nafasi moja hadi ya 18, sasa ikiizidi pointi mbili AFC Bournemouth inayoshika nafasi ya 19 na ina mechi moja mkononi, ikiwa mbele ya Norwich City yenye pointi 21 za mechi 35.
Samatta aliyejiunga na Aston Villa Januari mwaka huu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji, aliondolewa uwanjani dakika ya 80 kumpisha mshambuliaji chipukizi wa England, Keinan Davis.
Mabao ya Aston Villa leo yote yamefungwa na kiungo wa kimataifa wa Misri, Mahmoud Ahmed Ibrahim Hassan ‘Trezeguet’ dakika ya 45 na ushei na 59.
Crystal Palace ilipata pigo dakika ya 90 na ushei baada ya mshambuliaji wake, Christian Benteke aliyewahi kuchezea Aston Villa kutolewa kwa kadi nyekundu.
Kikosi cha Aston Villa kilikuwa; Reina, El Mohamedy, Konso Ngoyo, Mings, Taylor/Targett dk36, McGinn, Luiz, Hourihane/Nakamba dk80, Trezeguet/El Ghazi dk88, Samatta/Davis dk80 na Grealish.
Crystal Palace: Guaita, Ward, Dann, Sakho, van Aanholt, Zaha, Kouyate/Riedewald dk66, Milivojevic/Meyer dk75, McArthur/McCarthy dk46, Ayew/Townsend dk66 na Benteke.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇