Muwania kuombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Hai kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Saashisha Mafuwe akiwa amebebwa baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni ambapo wajumbe walimpigia kura 124
Na Dixon Busagaga, Hai
Mgombea ubunge katika jimbo la Hai katika kura za maoni za
Chama cha Mapinduzi (CCM) na kada wa chama hicho Saashisha Mafuwe ameibuka
mshindi baada ya kupigiwa kura 124 na wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo hilo.
Hatua hiyo ni hitimisho la chaguzi za ndani ya Chama cha Mapinduzi za kura za maoni katika ngazi ya majimbo
ambapo majimbo manne kati ya tisa ya mkoa wa Kilimanjaro yalikuwa yamesalia
baada ya zoezi hilo kuanza siku Jumatatu.
Majimbo yaliyokuwa yamesalia katika uchaguzi uliofanyika
Jumatatu ni pamoja na jimbo la Moshi vijijini,Jimbo la Hai na Jimbo la Same
Magharibi .
Katika uchaguzi wa jimbo la Hai Mafue ambaye ni mtumishi
kati tume ya madini amewashinda aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Hai Fuya Kimbita aliyepata kura 85 akifuatiwa na
Abubakar Msangi aliyepata kura 48 kati
ya wagombea 42 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
Katika Jimbo la Moshi vijijini wagombea walikuwa ni 47
waliorejesha fomu huku wagombea 46 wakijitokeza kuwania nafasi hiyo ,mpambano
mkali ukikua baina ya Prof Patrick Ndakidemi,Deogratius Mushi na Moris Makoye .
Msimazmizi wa uchaguzi katika jimbo la Moshi mjini Asia
Halamga akamtangaza Profesa Patrick Ndakidemi kuwa mshindi baada ya kuibuka kura
262 akiwashinda Deogratius Mushi aliyepata kura 46 akifuatiwa na Moris Makoi .
Katika jimbo la Same Magharibi ,Mbunge anayemaliza muda wake
Dkt Mathayo David ametetea nafasi yake baada ya kupata kura 389 dhidi ya kura
300 za mshindani wake aliyemfuatia Angela Kairuki huku nafasi ya tatu
ikishikiliwa na Marry Mgonja aliyepata kura 18.
Hatua ya awali ya uchaguzi katika majimbo ya mkoa wa
Kilimanjaro umemalizika huku majina ya walioshika nafasi za juu yakitaraji
kupelekwa katika vikao vya Chama cha
Mapinduzi kwa ajili ya mapendekezo na maamuzi .
Chama cha Mapinduzi kwa sasa kinajielekeza katika Chaguzi za
kura za maoni kwa Wabunge watakaotokana na viti maalumu zoezi linalotarajia
kufanyika siku ya Alhamisi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇